Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi akizungumza jambo leo jijini Dar es Salaam katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Idara ya afya wakiwemo wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, wawakilishi kutoka balozi mbalimbali, Madaktari bigwa, Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) wakiwa katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell nchini Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam (Picha Na Noel Rukanuga)
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe (wapili kutoka kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau idara ya Afya wakiwemo wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, wawakilishi kutoka balozi mbalimbali, Madaktari bigwa katika Kongamano la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha Na Noel Rukanuga)
…………………………………………………………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema ipo katika mpango mkakati wa kuhakikisha hospitali zote za Mikoa zinakuwa na kituo cha kupima na kutoa matibabu ya ugonjwa wa sickle cell pamoja na kuboresha sera jambo ambalo litasaidia kutokomeza ugonjwa huo.
Miongoni mwa maboresho ya sera katika idara ya afya ni kuhakikisha wachumba mwanamke na mwaume kabla ya kufunga ndoa wanapimwa vina saba ugonjwa wa sickle cell ili kukata mnyororo wa watoto kupata ugonjwa huo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la Kisayansi la kukabiliana na ugonjwa wa Sickle cell, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara ya Afya, Prof. Abel Makubi, amesema kuwa bado kuna tatizo kubwa la sickle cell, kwani takwimu zinaonesha kila mwaka tunapata wagonjwa 11,000 wanaozaliwa sickle cell.
Profesa Makubi amesema kuwa idadi hiyo ya 11,000 inaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano duniani zinazoongoza kuwa na ugonjwa wa sickle cell.
Amesema kuwa sickle cell inaitaji kufanyiwa mkakati maalum ili kupunguza uzito, huku akieleza kuwa nchi zinazoongoza kuwa na watu wengi wenye sickle cell duniani ni Liberia, Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo, Angola, India pamoja na Tanzania.
“Ugonjwa wa sickle cell unatokana na mtto kurithi vina saba vya sickle cell kutoka kwa wazazi wake wote wawili, hivyo mtoto anapozaliwa na sickle cell baba na mama wanakuwa wamechangia” amesema Profesa Makubi.
Profesa Makubi amebainisha kuwa takwimu zinaonesha kuwa asilimia 13 hadi 20 ya watanzania wana vina saba vya ugonjwa wa sickle cell, huku akieleza kuwa “Sickle cell umechangia asilimia saba vifo vyote vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kiwango ni kubwa na serikali hatuwezi kukaa kimya” amesema Profesa Makubi.
Amesema kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika zimeonesha kuwa ugonjwa wa sickle cell unapogundulika mapema na kupata matibabu inaongeza idadi ya siku za kuishi kwa mtoto na kupunguza idadi ya vifo pamoja na kulazwa hospitali mara kwa mara.
Ili kuepukana na ugonjwa sickle cell, serikali imeongeza huduma za maabara kwani awali huduma ya vipimo ilikuwa inapatikana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuleta usumbufu kwa wananchi.
“Kufika mwezi Disemba mwaka 2021 kila hospitali ya wilaya, kanda na hospitali binafsi zilionesha jitaida katika kuunga mkono katika kutoa huduma ya sickle cell” amesema Profesa Makubi.
Amesema ameshauri kuwa kabla ya mtu ajaowa anatakiwa kupata ushauri ili kupunguza uzito wa sickle cell na namna kuishi na mweza wake kama wakibainika wote wana vina saba vya sickle cell.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe, amesema kuwa katika jitiada wamefanikiwa kuongeza kliniki za kutoa huduma ya ugonjwa wa sickle cell katika hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Temeke, Amana na Mwananyamala.
Profesa Pembe ameeleza kuwa kuanzia mwaka 2016 wamefanikiwa kuongeza wigo wa kutoa huduma na kufika maeneo mbalimbali Mkoa wa Mwanza katika hospitali ya Bugando na Zanzibar, mnazi mmoja.
“Sekta binafsi ikiwemo hospitali ya Aghakan wanatoa huduma ya kliniki na tumeweka mpango mkakati wa kitaifa kuwa sickle cell kuwa katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo mpango huo unatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu” amesema Profesa Pembe.
Profesa Pembe ameishukuru serikali kwa ushirikiano katika kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa wa sickle cell hapa nchini.
Katika Kongamano hilo la kujadili mwelekeo wa ugonjwa wa sickle cell nchini Tanzania wadau mbalimbali wameshiriki wakiwemo wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, wawakilishi kutoka balozi mbalimbali, Madaktari bigwa ambapo mawazo yao yanakwenda kuboresha sera idara ya afya.
Sickle cell ni aina ugonjwa wa kurithi ambao huathiri cell nyekundu za damu na vibeba oxygen kwenye damu vinavoitwa haemoglobin. Kutokana na kwamba ugonjwa huu ni wa kurithi hiyvo unaweza kuambukizwa kupitia kizazi kimoja hadi kingine.
Ifahamike kwamba sickle cell ni aina mojawapo kati ya magonjwa ya siko seli lakini wenyewe huletekeza dalili mbaya zaidi na kuzorotesha afya ya mgonwa kama kuongezeka kwa maambukiz mbalimbali, homa ali na figo kushndwa kufanya kazi na matatizo mengine mengi kuliko aina zingine za siko seli.
Watu wengi wenye ugonjwa huu wa sickle cell seli hupata upungufu mkubwa wa virutubisho katika mwili kutokana na uwezo mdogo wa kufyonza viini lishe kutoka kwenye chakula anachokula.