Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikagua kitalu cha miche katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa ziara ya kukagua na kuhamasisha uhufadhi wa mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwanawisha maji wanafunzi wa Shule ya Misngi Magufuli baada ya kupanda mti ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Kampeni ya Soma na mti wakati wa ziara yake jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Misngi Magufuli baada ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Kampeni ya Soma na mti wakati wa ziara yake jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mayeka Simon Mayeka mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Misngi Magufuli (hawapo pichani) baada ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Kampeni ya Soma na mti wakati wa ziara yake jijini Mbeya.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
…………………………………………..
Na.Robert Hokororo, Mbeya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshauri halmashauri ziwatumie na ziwawezeshe vijana na wanawake katika kuanzisha vitalu vya miche kwa ajili ya kupandwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Ametoa ushauri huo leo Januari 25, 2022 alipotembelea kitalu cha miche katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za uhifadhi wa mazingira.
Dkt. Jafo alishauri halmashauri hizo zipanue wigo wa bajeti zao na kuviwezesha vikundi hivyo ili viweze kuotesha miche ili kusaidia kukutatua changamoto ya uhaba wa miche.
“Mnapokuwa na vikundi vya vijana wanaootesha miche kutasaidia kuhifadhi maqzingira na wakati huo watakuwa wanapata ajira kupitia biashara ya miche ambayo wataziuzia taaisisi na hata halmashauri zingine,” alisema.
Aliongeza kuwa inapendeza kuwa na majiji yaliyopandwa miti hasa ya matunda hatua itakayosaidia katika suala zima la uhifadhi wa mazingira na lishe wakati huo kupata matunda.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo alitembelea Shule ya Msingi Magufulu iliyopo jijini Mbeya ambapo alizindua Kampeni ya upandaji miti kwa wanafunzi wa shule na vyuo inayofahamika kama kampeni ya ‘Soma na Mti’.
Akiwa katika shule hiyo alipanda miti na wanafunzi hao huku akiwapongeza kwa kuweza kupanda miti ikiwa ni mojawapo ya hatua za kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kupanda miti.