Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sarah msafiri akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha mapinduzi.
…………………………………………………………….
Na Victor Masangu,Kibaha
Serikali Wilayani Kibaha mkoani Pwani imesema kwamba katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, fedha za miradi zilipokelewa kwa Mwaka 2021/2022 katika Halmashauri ya mji kibaha imepokea kiasi shilingi sh.894,659,920.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sarah Msafiri wakati wa kuzungumzia utekelezaji wa Chama ambapo amesema kati ya fedha hizo walizoporea RUWASA imepokea kiasi cha shilingi milioni 18,051,104.30.
“Aidha katika kutekeleza miradi mbali mbali pia kwa upande wa DAWASA imepokea kiasi cha shilingi 2,557,131,040 TARURA sh.1,097,822,898 na TANESCO sh.49,298,700,000 Jumla ikiwa ni sh.Bilioni 53,866,364,962.30,”alisema Msafiri.
Pia aliongeza kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha katika kutekeleza Ilani hiyo mpaka kufikia robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 kupitia vyanzo vyake vya ndani hadi kufikia tarehe 30 Disemba,2021 imeshakusanya sh.2,888,959,200 kati ya sh.4,107,012,000 sawa na asilimia 70.3.
Akizungumza Kuhusiana na utekelezaji katika miradi ya sekta ya Viwanda na Biashara Ilani ya Chama katika ibara yake ya 46 (g) imeweza kuelekeza juu ya kuandaa mikakati ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uanzishaji wa viwando vidogo,vya kati pamoja na vikubwa.
Hivyo mkuu huyo alibainisha kuwahivyo katika kutekeleza hilo Halmashauri ya Mji Kibaha imefanikiwa kuendelea na ujenzi wa Viwanda 15 kati yake vikubwa ni 4,vya kati ni 9 na vidogo vidogo 2 na hadi kufikia Disemba jumla ya Viwanda vikubwa ni 28,vya kati ni 23 na vidogo vidogo ni 9.
Akizungumzia katika miradi ya sekta ya afya wameweza kutekeleza ujenzi wa Kituo cha Afya Kongowe baada ya kupokea sh.250 milioni fedha za tozo kutoka Serikali kuu
aidha, hospitali ya Wilaya Lulanzi imeendelea kuboreshwa kwa kuongezewa majengo matatu ambayo ni wodi ya wanawake,wanaume na Watoto.
Kadhalika alisema kuwa katika miradi ya Sekta ya Elimu Sekondari Halmashauri ya mji kibaha imetekeleza ujenzi wa vyumba 47 vya Madarasa katika shule za Sekondari 13 baada ya kupokea milioni 940 za mpango wa Maendeleo wa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
“Tayari Madarasa yamekamilika na yameanza kutumika tangu tarehe 17 Januari 2022 na hii yote ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha mapinduzi ,”Sarah
Katika hatua nyingine alisema Halmashauri ya mji Kibaha imetekeleza ujenzi wa vyumba 47 vya Madarasa katika shule za Sekondari 13 baada ya kupokea milioni 940 za mpango wa Maendeleo wa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.