………………………………………………
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA WATANO KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA KWA KUWAKATA MAPANGA VICHWANI NA SHINGONI USIKU WA TAREHE 18/01/2022 MAJIRA YA 23:30 KUAMKIA TAREHE 19/01/2022 HUKO MAENEO YA MTO JELLYS MTAA WA MECCO KUSINI WILAYA YA ILEMELA.
WALIOUWAWA KATIKA TUKIO HILO WALITAMBULIKA KUWA NI:-
- MARRY CHARLES, MIAKA 42, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MECCO WILAYA YA ILEMELA (MAMA WA FAMILIA)
- 2. JENIFA FREDY @ NICE, MIAKA 22, MKULIMA, MKAZI WA MECCO KUSINI AMBAYE NI MTOTO WA MAREHEMU MARRY CHARLES NA
- MONICA JONAS, MIAKA 19, ALIYEKUWA NI MSAIDIZI WA KAZI ZA NDANI WA FAMILIA HIYO.
BAADA YA TAARIFA ZA TUKIO KUPOKELEWA, JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LILIANZA UPELELEZI WA KINA AMBAPO KUANZIA TAREHE 19/01/2022 HADI TAREHE 23/01/2022 JUMLA YA WATUHUMIWA WATANO WAMEKAMATWA WAKIWA NA VIELELEZO MBALIMBALI ZIKIWEMO MALI ZA MAREHEMU AMBAZO ZILIPORWA BAADA YA TUKIO NA ZIMEWEZA KUTAMBULIWA NA NDUGU WA MAREHEMU.
MALI HIZO NI:-
- FRIDGE AINA YA KYOTO,
- GODORO MOJA LENYE UKUBWA WA FUTI 4X6,
- TV MBILI AINA YA SINGSUNG ZOTE INCHI 18,
- RADIO MBILI (2) MOJA AINA YA SEAPIANO NA NYINGINE AINA YA ALPU,
- JIKO MOJA LA GESI AINA YA NIKLE NA
- SIMU TATU (3) AINA YA TECNO ZILIZOPATIKANA NYUMBANI KWA MMOJA WA WATUHUMIWA MAENEO YA BUHONGWA
KATIKA MAHOJIANO YALIYOFANYWA WATUHUMIWA WAMEKIRI KUTENDA TUKIO HILO. AIDHA SILAHA AINA YA PANGA LILILOTUMIKA KUTENDEA TUKIO HILO LIMEPATIKANA.
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NI:-
- THOMAS JILALA SONGAY, MIAKA 26, MSUKUMA MKOKOTENI, MKAZI WA MTAA WA UTEMINI-BUHONGWA
- HAJIR W/O THOMAS, MIAKA 23, FUNDI CHEREHANI, MKAZI WA BUHONGWA.
- DEOGLAS VICENT MALENGWA, MIAKA 31, MUUZA DUKA LA VIFAA VYA UMEME, MKAZI WA BUHONGWA
- EMMNAUEL CHARLES LUGAILA, MIAKA 36, KAZI YAKE NI OPERATOR WA MITAMBO KATIKA MGODI WA MWADUI, MKAZI WA MECCO KUSINI/ MWADUI.
- EMMANUEL MATHEW, MIAKA 19, MKAZI WA BUHONGWA.
WATUHUMIWA HAWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA KUKAMILISHA UPELELEZI WA TUKIO HILI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUWASAKA BAADHI YA WATUHUMIWA AMBAO BADO HAWAJAKAMATWA.
KIINI CHA TUKIO NI MGOGORO WA KIBIASHARA KATI YA MAREHEMU NA BAADHI YA WATUHUMIWA.
AIDHA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHUKURU WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KWA USHIRIKIANO WAO KATIKA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU. JESHI LINAZIDI KUTOA ONYO KWA WATU WENYE KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIHALIFU KUWA HAWATOWEZA KUKWEPA MKONO WA SHERIA.
IMETOLEWA NA;
RAMADHANI H. NG’ANZI- SACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.