Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango pamoja na mkewe mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki ibada ya Misa Takatifu dominika ya tatu ya mwaka C wa kanisa katika Kanisa Kuu katoliki la Bikira Maria Mshindaji Jimbo la Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Misa Takatifu dominika ya tatu ya mwaka C wa kanisa katika Kanisa Kuu katoliki la Bikira Maria Mshindaji Jimbo la Kigoma.
……………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiambatana na mkewe mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 23 Januari 2022 wameshiriki ibada ya Misa Takatifu dominika ya tatu ya mwaka C wa kanisa katika Kanisa Kuu katoliki la Bikira Maria Mshindaji Jimbo la Kigoma. Misa hiyo imeongozwa na Askofu wa Jimbo la Kigoma Joseph Roman Mlola.
Makamu wa Rais ametumia Misa hiyo kuwashukuru waumini,wananchi wa Kigoma pamoja na watanzania kwa ujumla waliompa faraja yeye pamoja na familia kufuatia kifo cha kaka yake Askofu mstaafu wa kanisa la Anglikana Gerald Mpango.
Aidha amewasihi waumini pamoja na viongozi wa kanisa hilo kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wake ili kudumisha Amani na utulivu hivyo kuendelea kumtukuza Mungu katika mazingira salama.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewapongeza waumini wa Kanisa Kuu la Bikira Maria Mshindaji Jimbo la Kigoma kwa kujitoa katika kukamilisha kanisa hilo ambalo litatumika kumtukuza Mungu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Makamu wa Rais ameendesha harambee kwa wasaidizi wake waliokuwepo kanisani hapo na kukusanya kiasi cha shilingi milioni moja laki tatu na elfu thelathini na nne ambazo amezikabidhi kwaajili ya maendeleo ya kanisa hilo.