***********************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba Sc imeshindwa kupata matokeo mazuri kwa mara nyingine tena mara baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro.
Simba Sc ambayo katika mchezo huo walicheza kwa dakika 45 kipindi cha kwanza wakiwa wanatawala mchezo huo na kukosa nafasi nyingi za wazi kupitia kwa washambuliaji wao ambao walionekana kabisa walizidiwa umakini na mabeki wa Mtibwa Sugar ambayo safu ikiongozwa na Abdi Banda beki wa zamani wa Simba Sc.
Mtibwa Sugar walionekana kushambulia kwa kushtukiza wakiwa wanausoma mchezo na kuweza kuwakamata Simba Sc ambao walionekana dhahiri wanahitaji ushindi lakini wachezaji wa Mtibwa walionekana kutofurahishwa na Simba Sc kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo.
Pengine ugumu wa mechi hii unatokana na ubovu wa uwanja ambao ulijawa na maji ya mvua.
Simba Sc sasa itawafuata tena Kagera Sugar Jumanne hii katika uwanja wa Kaitaba kumalizia kiporo cha mchezo huo.