Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasili kushiri katika viwanja vya Chuo cha Ushiriki Moshi kwaajili ya kushiriki katika Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro lililofanyika leo Januari 22,2022 Mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassani akizungumza katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Mhe.Paulina Gekul akitoa hotuba yake katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lilofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 na kuhudhuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye pia alikuwa mgeni Rasmi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Steven Kigaigai akitoa hotuba yake katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lilofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 na kuhudhuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye pia alikuwa mgeni Rasmi.
Baadhi ya Machifu Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika Tamasha la Utamaduni mkoa wa Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. Tamasha hilo limefanyika leo Januari 22,2022 katika Viwanja vya Chuo cha Ushiriki Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya viongozi wa Dini Mkoa wa Kilimanjaro wakishiriki Tamasha la Utamaduni mkoa wa Kilimanjaro ambalo limefanyika leo Januari 22,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani humu ambapo Mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan akivalishwa vazi la Utamaduni kama ishara ya kukaribishwa katika mkoa wa Kilimanjaro katika Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika leo tarehe 22/01/2022 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa ngao na mkuki na baadhi ya machifu wa Mkoa Kilimanjaro katika Tamasha la Utamaduni lililofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassani akipata picha ya pamoja na baadhi ya machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO,KILIMANJARO
………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewapa pole wananchi wa mkoa Kilimanjaro na mikoa mingine kutokana na ukame ulioikumba mikoa hiyo hususan katika maeneo ya ufugaji uliosababishwa na kuchelewa kunyesha kwa mvua na hivyo kupelekea wananchi kupoteza maelfu ya mifugo yao.
Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 22 Januari, 2022 Moshi mkoani Kilimanjaro wakati uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni Kilimanjaro lililoandaliwa na uongozi wa Machifu wa mkoa huo.
Mhe. Rais Samia amewataka wafugaji kushirikiana na Serikali ili kutumia mafunzo waliyoyapata kutokana na janga la ukame kuona namna bora ya kuanza ufugaji wa kisasa usiotegemea mvua katika kupata malisho.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewashukuru Machifu wa mkoa huo kwa kuitikia wito alioutoa mkoani Mwanza na kuelekeza mikoa yote nchini kufanya matamasha ya utamaduni kwa lengo la kuendeleza mila, desturi na utamaduni wa taifa letu ili zisipotee.
Mhe. Rais Samia amesema Serikali iliunda Wizara mahsusi itakayosimamia moja kwa moja shughuli za sanaa, utamaduni na michezo kwasababu ilitambua umuhimu wa sekta hizi katika kutoa ajira, kukuza uchumi wa nchi na kuitangaza nchi kimataifa.
Vile vile, Mhe. Rais Samia ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kuratibu, kuvikuza na kuviendeleza vikundi vya burudani za kitamaduni ili vizalishe kazi za mikono za utamaduni kama vile ufinyanzi, ususi, upishi, uchongaji pamoja na kuhamasisha mashindano ya tambo, tenzi, nahau na ushairi kwa kutumia mila na usarifu wa lugha ya Kiswahili.
Mhe. Rais Samia amezitaka Wizara zinazoshughulikia utamaduni na utalii kuandaa mkakati wa pamoja wa kuyabaini matamasha ya kimataifa na kimkoa yatakayoboreshwa na kuendeshwa kimkakati ili yaweze kuwavutia wageni kutoka nje na ndani ya nchi na kuitangaza nchi yetu.
Katika kuendeleza na kuimarisha utamaduni, mila na desturi za kitanzania, Mhe. Rais amesema tayari Serikali imeanzisha kanzi data sahihi inayohusu Machifu, na kwamba Serikali imeanza kuweka taarifa sahihi za Machifu na mchango wao katika kupambana na ukoloni.
Mhe. Rais Samia pia amesema kuwa Serikali inaendelea kuyabaini maeneo ya kichifu na kimila na kuyatunza ili yawe sehemu za vivutio vya nchi yetu pamoja na kuibua, kuimarisha na kuhifadhi majengo na zana za zamani ili zibaki kuwa vielelezo vya utamaduni wetu.
Aidha, Mhe. Rais Samia amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Maliasili na Utalii zinaendelea na majadiliano ya urejeshwaji wa mafuvu ya Machifu yaliyochukuliwa wakati wa ukoloni ili yatumike kuelimisha jamii.
Mhe. Rais Samia amewasihi viongozi wa Machifu kuwahimiza watanzania kujilinda na janga la UVIKO 19 ikiwa ni pamoja na kupata chanjo na kuwahamaisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa litakalofanyika mwezi Agosti mwaka 2022.
Katika Tamasha hilo Mhe. Rais Samia ametembelea mabanda ya makabila matatu ya Wachaga, Wapare na Wamasai na kuonesha vitu mbalimbali ikiwemo vyakula vya asili vya makabila hayo pamoja na dawa za asili.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.