Na John Walter-Mbulu
Serikali imesema imeweka mazingira ya usawa kwa wanafunzi wote wa mijini na vijijini, katika utoaji wa kompyuta kwenye shule mbalimbali za sekondari nchi nzima, Ili kuwaandaa wanafunzi kuelewa matumizi sahihi ya TEHAMA, yatakayowawesha kutafsiri fursa zilizopo katika jamii.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Habari Mawasiliano na teknolojia ya mawasiliano, Mhandisi Kundo Andrea Mathew, January 20/2022, akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
Kundo amesema serikali imetenga Bilioni 45 kwa ajili ya kuhakikisha mfumo wa anuani za makazi unawekwa nchi nzima ambazo zitawasaidia kufanya biashara za mitandaoni, pamoja na wananchi kufikiwa na huduma mbalimbali kutoka maeneo mengine Hadi mahali walipo.
Akizungumzia changamoto kubwa inayowakabili wananchi, Mbunge wa Jimbo la Mbulu vijijini Flatery Massay, Amesema changamoto ya mawasiliano imekwamisha mambo mbalimbali, pia amewataka wananchi kuanza kununua simu kwani changamoto hiyo itatuliwa hivi karibuni na serikali.
Minara hiyo inayojengwa imefadhiliwa na mfuko wa mawasiliano kwa wote na wamejikita katika maeneo ya vijijini na baadhi ya maeneo ya mijini, ambapo Kuna usikivu hafifu wa mawasiliano, kwa kutoa ruzuku kwenye makampuni ya mitandao ya simu ili wapeleke huduma ya mawasiliano kwa wananchi, pamoja nakupeleka mawasiliano ya redio katika maeneo ambao Kuna usikivu hafifu wa redio.