Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba akizungumza katika ziara hiyo.
Kamati hiyo ikikagua ujenzi wa Shule Shikizi ya Kisingi iliyopo Kata ya Kitukutu. wilayani Iramba.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda akisisitiza jambo kwenye ziara hiyo. kutoka kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Shee, Mjumbe wa siasa mkoa wa Singida, Diana Chilolo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Singida Dk.Devis Nyiraha.
Taarifa ya ujenzi wa madarasa mawili ya Shule Shikizi ya Kisingu ilitolewa (kushoto) ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Singida, Yusuph Mwandami.
Ukaguzi wa ujenzi wa Shule Shikizi ya Isingu ukiendelea.
Muonekano wa moja ya majengo ya Shule ya Sekondari ya Kinambeu iliyopo wilayani Iramba.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kinambeu Godfrey Yohana akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo.
Muonekano wa madara mawili yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Nduguti wilayani Mkalama.
Muonekano wa Kituo cha Afya Ilunda kinachoendelea kujengwa.
Ziara ikiendelea.
Taarifa ya mradi wa maji wa Kijiji cha Nkungi ikitolewa na Mhandisi anaye jenga mradi huo. |
Muonekano wa tenki la maji la mradi huo. |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkalama Lameck Itungi (kulia) akizungumza katika ziara hiyo. Anayetabasamu wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Shee akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Nkungi.
Katibu wa Iguguno Youth Group Winfrida Innocent (kushoto) akitoa taarifa kwa wajumbe wa siasa Mkoa wa Singida wakati wa ziara hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imezipongeza Halmashauri za Wlaya ya Mkalama na Iramba kwa kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati kamati hiyo ikikagua miradi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa , Alhaji Juma Kilimba alisema ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo katika halmashauri hizo.
“Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza hasa ujenzi wa madarasa yalitokana kwa fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19,” alisema Kilimba.
Kilimba alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza kutokana na umuhimu wake.
Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.
Kilimba alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo ambayo kwa mkoa mzima zimetumika Sh.13.4 Bilioni kumewaondolea adha ya kusoma katika mazingira yasiyo rafiki kwa wanafunzi kuanzia shule shikizi, msingi sekondari na akataka miradi hiyo kutunzwa.
Alisema hivi sasa nchini kote baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kazi kubwa ya kutoa fedha hizo wananchi hawazungumzii tena ujenzi wa madarasa au ukosefu wa madawati kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na kuwa nguvu inaelekezwa kuhimarisha mitaala.
Aidha Kilimba aliwataka wataalamu wa halmshauri mbalimbali kutoa mafunzo kwa vijana wanaokopeshwa fedha na halmashauri kupitia asilimia 10 kwa lengo la kuwafanya kuwa na uwezo wa kuendesha miradi hiyo akiutolea mfano mradi wa Iguguno Youth Group ambao unajishughulisha na ufugaji wa kuku na ufyatuaji wa matofali.
Alitumia nafasi hiyo kuziomba halmashauri za wilaya kutoa kazi kwa vikundi vya vijana ili kuviinua kiuchumi na kukuza mitaji yao.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace amewapongeza mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu kwa kutekeleza kwa umakini wa hali ya juu kufanya kazi nzuri ya kusimamia ujenzi wa madarasa hayo kama alivyotaka Rais Samia Suluhu.
Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza wakuu wa shule na viongozi waliosimamia fedha za kutekeleza miradi hiyo kwa kuwa waaminifu na kufanikisha miradi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda akizungumzia ujenzi wa Shule Shikizi ya Kisingu iliyopo Kata ya Kitukutu alisema walipokea fedha za ujenzi wa madarasa ambapo awali uwezo wa kupokea wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza walikuwa 2,800 ambapo mwaka jana walikuwa ni 3,211 hivyo kulazimika kutumia majengo ya maabara na wanafunzi 466 walipelekwa kwenye madarasa hayo kutokana na kutokuwa na madarasa ya kutosha.
Mwenda alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha hizo na kufanikiwa kujenga madarasa 47 ambayo yanauwezo wa kupokea zaidi ya wanafunzi 1,200 na kwa mwaka huu wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza walikuwa ni 4,022 ambao ni ongezeko la wanafunzi 800 na kuwa bila ya kujengwa kwa madarasa hayo wanafunzi 1200 walikuwa hawana sehemu ya kusomea lakini kutokana na msaada huo wa Rais wanafunzi wote wamepata madarasa ya kusomea na kubakia na ziada ya wanafunzi 80.
Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na watendaji wote wa wilaya kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miradi hiyo na kuwa mafanikio hayo yametokana kwa sababu ya kuwepo kwa ushirikiano.
Baadhi ya miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo katika Wilaya ya Iramba ni mradi wa maji uliopo Kata ya Maluga, ujenzi wa madarasa mawili ya Shule Shikizi ya Kisingu pamoja na ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Sekondari ya Kinambeu yaliyo jengwa kwa gharama ya Sh.60 Milioni.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo aliitaja baadhi ya miradi iliyotembelewa na kamati hiyo kuwa ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Nduguti ambavyo viligharimu Sh.40 milioni, ujenzi wa Kituo cha Afya Ilunda ambao umetumia Sh.250,000,000 fedha zilizotokana na tozo ya miamala ya simu, ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Nkungi ambao umegharimu Sh.444,000,000. Milioni na mradi wa Kikundi cha Iguguno Youth Group ambacho kinajishughulisha na ufugaji wa kuku na ufyatuaji wa matofali ambao wamewezesha mkopo na halmashauri hiyo.
Ziara hiyo iliwahusisha viongozi na wataalamu mbalimbali wa wilaya hizo pamoja na wakuu wa wilaya hizo