Jaji Mfawidhi Mahakama ya Morogoro Mheshimiwa Paul Ngwembe akifungua Mafunzo ya Hakimiliki kwa Mahakimu (hawapo pichani) leo Januari 20, 2022 Mkoani Morogoro, wakwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Doreen Anthony Sinare. Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Doreen Anthony Sinare akishukuru Taasisi ya Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kufanikisha ushiriki wa Mahakimu katika Mafunzo ya Hakimiliki yaliyoandaliwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Leo Januari 20, 2022 Mkoani Morogoro.
Jaji Mfawidhi Mahakama ya Morogoro Mheshimiwa Paul Ngwembe aliyekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu waliyoshiriki Mafunzo ya Hakimiliki yaliyoandaliwa na Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Januari 20, 2022 Mkoani Morogoro mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo, wa kwanza kulia aliyekaa ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Doreen Anthony Sinare.
Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania Lupakisyo Mwambinga akitoa mafunzo ya Hakimiliki kwa Mahakimu wa Tanzania (hawapo pichani) yaliyofanyika leo Januari 20, 2022 Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Mahakimu wakifuatilia Mafunzo ya Hakimiliki yaliyokuwa na tolewa na Mheshimiwa Jaji Dkt. Adam Mambi hayupo pichani leo Januari 20, 2022 Mkoani Morogoro, mafunzo hayo haya imeandaliwa na Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA).
Jaji Mfawidhi Mahakama ya Morogoro Mheshimiwa Paul Ngwembe (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa Mafunzo ya Mahakimu Tanzania mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili Mkoani Morogoro, wakwanza kulia aliyekaa ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Doreen Anthony Sinare, leo Januari 20, 2022, mafunzo hayo yameandaliwa na COSOTA.
******************************
Na Anitha Jonas – COSOTA, Morogoro
20/01/2022
Jaji Mfawadhi Mahakama ya Morogoro Mheshimiwa Paul Ngwembe aipongeza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)kwa kuandaa mafunzo ya Hakimiliki kwa Mahakimu asisitiza mafunzo hayo yataboresha uendeshaji wa mashauri ya uvunjifu wa hakimiliki.
Mheshimiwa Jaji Mfawidhi Ngwembe ametoa pongezi hizo leo Januari 20, 2022 Mkoani Morogoro alipokuwa akifungua Mafunzo hayo kwa Mahakimu yaliyoandaliwa na COSOTA kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Mahakama Lushoto ambayo yataendeshwa kwa siku mbili.
” Tunafahamu sasa dunia inakwenda katika kipindi cha nne cha mabadiliko ya viwanda na hapa kuna kazi nyingi za ubunifu zinajitokeza na biashara nyingi zinaenda kufanyika kwa njia ya mtandao, ni jambo zuri kuwajengea uwezo watendaji hawa wa shughuli za Mahakama sababu itarahisisha uendeshaji wa mashauri ya hakimiliki,” alisema Jaji Ngwembe.
Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Jaji Mfawidhi huyo alisisitiza kuwa wabunifu wote na wanakiwa kusajili kazi zao COSOTA ili kupata umiliki wa kazi na kuondoa mgogoro wa kumtambua mmiliki halali pale wanapoleta shauri mahakamani.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Doreen Anthony Sinare aliishukuru Taasisi ya Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana vyema na COSOTA kufanikisha mafunzo hayo kwa Mahakimu.
” Hivi sasa Serikali inasisitiza usimamizi wa haki za wasanii na wabunifu ili waweze kunufaika na kazi zao na ndiyo maana tumeona ni vyema tufanye mafunzo haya kwa Mahakimu ili mashauri ya Hakimiliki yanapofika mahakamani yaweze kuendeshwa kwa uelewa mzuri na kwa urahisi zaidi,” alisema Doreen.
Halikadhalika kwa upande wa moja wa washiriki wa mafunzo hayo Hakimu Mkazi kutoka Mahakama ya Kinondoni Denis Mshamu alieleza kuwa katika siku mbili hizo mbili za mafunzo anatarajiwa kujifunza mengi na kujijengea uelewa mzuri katika masuala ya Hakimiliki katika uendeshaji wa mashauri ya Hakimiliki mahakamani.
Aidha, mafunzo hayo yamefanikishwa kwa udhamini wa Multichoice Tanzania (DSTV) na Azam Media, vilevile zaidi ya Mahakimu thelathini na tano wameshiriki mafunzo hayo.