WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza na watendaji wa RUWASA wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa Mikataba ya ununuzi wa pampu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa bajeti ya mwaka 2021-2022 iliyofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo,akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa Mikataba ya ununuzi wa pampu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa bajeti ya mwaka 2021-2022 iliyofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wakifatilia hotuba ya wa Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa Mikataba ya ununuzi wa pampu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa bajeti ya mwaka 2021-2022 iliyofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo (kulia),akibadilishana Mkataba na Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Orgentum International Bi.Rose Jamese huku Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akishuhudia utiaji saini wa Mikataba ya ununuzi wa pampu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa bajeti ya mwaka 2021-2022 iliyofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo (kulia),akibadilishana Mkataba na Meneja Mauzo kutoka African Power Machinery Tanzania huku Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akishuhudia utiaji saini wa Mikataba ya ununuzi wa pampu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa bajeti ya mwaka 2021-2022 iliyofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkurugenzi kutoka Tribute Energy Bw.James Masaga,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa Mikataba ya ununuzi wa pampu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa bajeti ya mwaka 2021-2022 iliyofanyika leo Januari 20,2022 jijini Dodoma.
…………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Maji Juma Aweso,ameagiza kuanzia sasa pampu zifungwe katika maeneo yanayotoa maji hata kabla ya kujengwa kwa matanki ili wananchi waanze kunufaika kuliko kusubiri kwani kumekuwa kunachukua muda mrefu kukamilika.
Pia ameiagiza Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA), kuhakikisha kuwa miradi yote ya maji inakamilika kwa wakati na wale wote wanaofanya miradi hiyo kuhakikisha wanalipwa kwa wakati kwani huu si wakati wa kuweka maneno kwenye miradi ya maji bali iwe ni vitendo zaidi ili serikali ijivunie kufanya kazi na wakandarasi wazawa.
Waziri Aweso,ametoa maagizo hayo leo Januari 20,2021 Jijini Dodoma wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ununuzi wa pampu za maji 301, zinazolenga kufungwa katika mikoa mbalimbali nchini.
Mkataba huo umesainiwa kati ya Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) na wazabuni Wazawa kampuni nne moja ikiwa na kandarasi mbili ambapo Sh. 8.89 bilioni zitatumika kununua mashine pampu hizo
Amesema ili kuleta ufanisi katika miradi ya maji ambayo imetumia kiasi kikibwa cha fedha zilizotolewa katika awamu hii ya sita anapanga kuitisha kikao kati ya wizara hiyo na makandarasi wanaotekeleza miradi ya maji nchini.
“Mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu tutafanya kikao na makandarasi wote kwakuwa wao wana yao ya kutueleza katika changamoto zao lakini na sisi serikali tunayetu ya kuwaeleza lengo likiwa ni kufanikisha kuwafikishia huduma watanzania wote katika maeneo yote”amesema
Pia, amewataka wazabuni wa miradi ya maji kufanya kazi kwa muda na kuzingatia makubaliano ya mkataba husika kwani Watanzania wanataka maji siyo siasa.
Amesema hatakuwa tayari kuendelea kuona wananchi wanakunywa maji kwa kuchangia na punda wakati serikali tayari imetoa fedha za miradi ya maji kwa wakati.
Amesema akiwa Waziri mwenye dhamana ya maji hatakuwa tayari kuendelea kuona wananchi wanakunywa maji kwa kuchangia na mifugo wakati serikali tayari imetoa fedha nyingi kwa ajli ya miradi ya maji.
“Hatutakuwa tayari kuona mwananchi anaendelea kunywa maji na punda ili hali fedha za miradi ya maji tumepata kwa wakati”alisema Aweso
Amesema Serikali ya awamu ya sita inalengo la kumtua mama ndo kichwani kwa kuboresha miundombinu ya maji pamoja na kuanzisha vyanzo vipya vya maji.
“Niwaagize Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira vijijini Ruwasa, kuhakikisha kuwa miradi yote ya maji inakamilika kwa wakati lakini pia kwa wale wote wanaofanya miradi hii wakikamilisha walipwe kwa wakati asiyefanya kazi na asile”amesema Aweso.
Pia ameiagiza Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA), kuhakikisha kuwa miradi yote ya maji inakamilika kwa wakati na wale wote wanaofanya miradi hiyo kuhakikisha wanalipwa kwa wakati kwani huu si wakati wa kuweka maneno kwenye miradi ya maji bali iwe ni vitendo zaidi ili serikali ijivunie kufanya kazi na wakandarasi wazawa
Mkurugenzi wa Ruwasa Clement Kivegalo, alisema wazabuni waliopewa kazi hiyo watafanya kwa wakati kwa kuwa malipo na stahiki zote katika tenda hiyo zimekuwa tayari kinachoangaliwa ni kazi tu.
Kivegalo, amesema namna ilivyo sasa kilio cha maji kinakwenda kuwa historia katika nchi lakini akasisitiza usimamizi wa karibu wa miradi ili iwe na ubora na thamani ya fedha.
Mkurugenzi huo alimhakikishia waziri kuwa Ruwasa itafanya kazi usiku na mchana na karibu na wazabuni na makandarasi bila kuchoka hadi waone wanatimiza ndoto ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtoa mwanamke ndoo kichwani.
Akizungumza kwa niaba ya wazabuni James Masage , kutoka kampuni ya Tributa Energy, amesema hakutakuwa na kikwazo ikiwa watapewa malipo ya kazi zao kwa wakati.