********************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga Sc leo imeshuka dimbani katika mechi ya kirafiki akicheza na timu ya Mbuni Fc kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Kwenye mchezo huo Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0, mabao yote yakiwekwa kimyani na kiungo raia wa Dr Congo Mukoko Tonombe.
Mukoko ambaye usajili wake kwenda TP Mazembe kukwama leo hii alipewa nafasi ya kucheza kwa kwa dakika 90 na kuiwezesha timu yake kuondoka na ushindi ambapo mabao yote alifunga kwa Penati.
Yanga Sc iliwapa nafasi wachezaji wake wapya na ambao hawapo katika kikosi cha kwanza ili kuweza kumshawishi kocha na kuwajumuisha kwenye kikosi cha kwanza.
Yanga Sc iliwaanzisha wachezaji Johora, Paul Godfrey,Bryson, Bacca, Mukoko, Sureboy,Ambundo,Kaseke, Faridi na Makambo.