………………………………………………………
Na Lucas Raphael,Tabora
SERIKALI wilaya ya Tabora mjini imesema imetenga na itapeleka fedha kwenye miradi yote iliyofikia hatua ya boma ambayo yalikosa fedha kwa muda Fulani ili ikamilishwe.
Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Dk Yayha Nawanda alisema hayo wakati akiongea na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri wilaya (DCC).
Dk Nwanda alisema yapo maboma ambayo ya serikali kama vyumba vya mafarasa,zahanati na vituo vya afya,nyumba za walimu na majengo ya utawala ambayo yalisimama kutokana na kukosekana kwa fedha.
Alisema fedha zimetengwa tayari na sasa kata zote ambazo kuna miradi iliyosimama itakamilishwa kwa wakati sanjari na uwekaji wa samani.
Aidha,mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa hivi karibuni amepanga kufanya ziara kwa vijiji vyotevilivyo ndani ya wilaya yake na atakutana na wananchi ili kujua na kutatua kero zinazowakabili na kuzitatua.
Aliongeza kuwa amekuja wilaya ya Tabora mjini kuwa mkuu wa wilaya kusaidia wananchi anaowaongoza na siyo mkuu wa wilaya wa kukaa ofisini tu.
Hata hivyo aliwafahamisha wajumbe wa kikao cha (DCC) kuwa wilaya inakwenda vyma katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na mwaka ujao wa fedha wilaya haitapata hati chafu na hili linawezekana na wamejipanga vyema.
Katika hatua nyingine alisema wilaya imejipanga na kutenga fedha kwa ajili ya barabara ikiwemo uwekaji wa taa za kuongoza gari,pikipiki na waenda kwa miguu katika kata ya Malolo na eneo la Mwafrika.
Dk Nawanda aliwaomba viongozi wa vyama vya upinzani kujenga tabia ya kufika ofisni kwake ili kujadiliana mambo mbalimbali ya na kushauriana mambo ya maendeleo kwani Tanzania ni nchi watanzania wote.
Aidha,alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuja Tabora kuwa mkuu wa wilaya na kusema hatamuanguusha na atachapa kazi na kutekeleza ilani ya uchaguzi.
Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa Tabora Ramadhani Kapera alipongeza kazi kubwa inayofanywa na serikali ikiwemo fedha zinazotengwa kwenye miradi ya maendeleo kwani manispaa Tabora imeletewa fedha kiasi cha bilioni 2.9
Kapera alisema wao kama viongizi watazisimaia fedha hizo ili zilete tija kwenye miradi iliyokusudiwa na kuleta faida kwa wanatabora.