MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Tanga (CCM)Meja Mstaafu Hamis Mkoba akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa na kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga |
Katibu wa CCM wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Wajumbe wa kamati ya Siasa wilaya ya Tanga wakipata maelezo kuhusu mradi wa Maji wakati wa ziara hiyo
Wajumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Tanga na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakingia kwenye eneo la Machimbo ya Kokote
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa katika akitoka kwenye eneo hilo akiwa na Naibu Meya wa Jiji la Tanga Calvas Joseph kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga Ngonyani
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Tanga (CCM)Meja Mstaafu Hamis Mkoba amewataka watendaji wa serikali kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwa kuzingatia muda uliopangwa.
Aliyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga ya kukagua miradi ya Maendeleo Jijini Tanga huku akiwataka watendaji hao wabadilike waende kulingana ma kasi ya Rais Samia katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kwa kuzingatia fedha iliyotumika inaendena na mradi husika.
Alisema katika ziara hiyo wamebaini changamoto katika maeneo machache ilikuwepo ni usimamizi mdogo katika baadhi ya miradi michache waliyoikagua huku wakiipongeza Halmashauri ya jiji la Tanga kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa na ubora miradi mbalimbali niseme tu itoshe kuwa ni Halmashauri ya mfano na ya kuigwa nchini.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliwataka viongozi jijini Tanga wahakikishe miradi inayotekelezwa inazingatia ubora na matumizi sahihi ya fedha wanazopatiwa ili kuleta matokeo ambayo Rais amekusudia pia amewataka waone umuhimu na wajibu wa viongozi wa chama wakati wa kukagua miradi mbalimbali.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamis Mkoba,Mstahiki Meya wa jiji hilo Abdulrahman Shiloo, Naibu Meya wa Jiji hilo Colvas Joseph wakiwemo viongozi mbalimbali wa chama pamoja na watendaji wa serikali.
Alisema lazima viongozi wa chama na watendaji wa halmashauri kufanya ukaguzi mara kwa mara katika miradi inayotekelezwa ili kuleta tija kwa wananchi na hatimaye kuweza kuwa chahu ya maendeleo
Mgandilwa alisema serikali imekuwa ikitumia gharama nyingi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo ni wajibu wa viongozi kuhakikisha fedha zinazotolewa zinalingana na miradi inayotekelezwa.
Aidha Mgandilwa aliwakumbusha viongozi na watendaji wa halmashauri ya jiji pamoja na taasisi zingine kuhakikisha fedha yeyote inayoletwa na serikali iweze kuleta matokeo ambayo Rais amekusudia.
Alisema kwa sababu kuna maeneo mengine unaweza ukaenda ukakuta gharama iliyotumika ni kubwa ukilinganisha na uhalisia hivyo ukipima value for money huwezu kuipata hivyo serikali hii ya awamu ya 6 chini ya Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan anatoa wito mara kwa mara na kusisitiza kwamba ni vyema watendaji wote tuendelee kusimamia matumizi sahihi ya fedha.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amesema ziara hiyo wameifanya kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kuanzia mwezi July-Desemba 2021.
Meya Shiloo amesema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni namna gani ilani ya chama inavyotekelezwa lakini pia kuona mapungufu katika utekelezaji wa ilani na kujua hatua za kuchukua.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ya, siasa ni pamoja na miradi ya elimu, afya,