Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwasili katika Hafla ya kutunuku vyeti kwa Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo katika Chuo cha Hoteli na Utalii VETA Njiro
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika hafla ya kutunuku vyeti kwa Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo katika Chuo cha Hoteli na Utalii VETA Njiro
Baadhi ya wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo wakipongezwa na Waziri wa Elim, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda baada ya kuimba shairi.
Mmoja wa Wahitimu wa Programu ya Uanagenzi akitoa ufafanuzi wa kile walichojufa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu wakifurahia jambo wakati wa Hafla ya kutunuku vyeti kwa Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo katika Chuo cha Hoteli na Utalii VETA Njiro
…………………………………………………………….
Na WyEST,Arusha
Serikali kufanya tathimini ya wahitimu wanaomaliza katika Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ili kuona namna wanavyoweza kujiajiri ama kujiajiriwa baada ya kumaliza mafunzo
Kauli hiyo imetolewa leo Januari,15 2022 jijini Arusha na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda katika hafla ya kutunuku vyeti Wanagenzi wahitimu wa Mpango wa Urasilimishaji Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi ambapo amesema mafunzo yanayotolewa ni lazima yaendane na ujuzi unaotakiwa katika soko ajira.
Prof. Mkenda amesema pamoja na kuangalia wahitimu hao wanafanya kazi gani ama wamejiajiri wapi pia Wizara inatarajia kuangia mtazamo wa waajiri wa wahitumu hao na kuwataka kutoa ushauri nini kiongezwe katika mafunzo na kipi kiwekewe mkazo ili kuwezesha VETA kutoa mafunzo yenye tija kwa vijana na Taifa.
” Tunatoa mafunzo ya VETA kwa sababu tunataka kuongeza ujuzi kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika na sio suala la idadi kwamba tunatoa vyeti kwa wahitimu wangapi au tunajenga vyuo vingapi, tunataka tuone ujuzi na taaluma wanayoipata inatumika. Tunataka Waajiri waanze kuulizia watu wenye vyeti vya VETA” amesisitiza Waziri huyo
Waziri huyo ameongeza kuwa hata ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka kuongezwa kwa ajira mpya milioni nane ifikapo 2025, hivyo vijana wanaosoma VETA wakifundishwa vizuri na kupata ujuzi stahiki wataajirika na itasaidia kuondoa mazoea ya sasa ya waajiri kutafuta wafanyajazi nje ya nchi.
Aidha Prof. Mkenda amewataka wahitimu wa programu ya uanagenzi kutokubweteka katika hatua waliofikia ila waendelea kujisomea zaidi kwani mafunzo hayo yamewafungulia jukwaa la kupata elimu zaidi ili kuwawezesha kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea Duniani
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amesema lengo kuu ya programu ya Taifa ya kukuza ujuzi ni kuwezesha nguvu kazi ya taifa kupata ujuzi na stadi za kazi ili kumudu ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Prof. Ndalichako amesema washiriki ambao wamehitimu wamepata mafunzo kwa kuzingatia mapungufu yaliyojitokeza wakati wanafanyiwa tathimni kutokana na ujuzi walio nao hivyo mafunzo na vyeti walivyopota vitawawezesha kujiendeleza kielimu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kaspar Mmuya amesema mafunzo hayo kwa awamu tatu yameshatoa zaidi ya wahitimu elfu 20 ambao ujuzi wao umerasilimishwa na kupatiwa vyeti.