NAIBU Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli,akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC), Pauline Nkwama,akielezea jinsi walivyojifunza mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Mratibu Elimu TAMISEMI Bw.Richard Makota,akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Nchini Bi.Germana Mung’aho,akitoa neno la shukrani kwa niaba kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde (hayupo pichani) mara baada ya kufunga mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa,Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda yaliyofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
…………………………………………………………….
Na Alex Sonna, Dodoma
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde, amewataka Wasimamizi wa walimu, kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wanahudhuria darasani kila siku kulingana na ratiba za masomo zilizvyopangwa ili kuepuka kuathiri utekelezaji wa Kalenda ya mitaala.
Silinde ametoa kauli hiyo leo Januari 15,2022 jijini Dodoma wakati akifunga Mafunzo ya kalenda ya utekelezaji wa mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa Maafisa Elimu Mikoa, Maafisa Taaluma Mikoa na Wathibiti Wakuu wa Ubora wa Shule Kanda.
Amesema hatua hiyo itasaidia utekelezaji wa Kalenda hiyo.
Aidha, amesema Kalenda ya Utekelezaji wa Mitaala inakwenda sambamba na upatikanaji na matumizi sahihi ya vitabu vya kiada na ziada.
“Naamini kuwa Shule zote zina vitabu vya kutosha na vingine vinaendelea kusambazwa na Taasisi ya Elimu Tanzania. Naomba kuwakumbusha kwamba vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi, huvitumia kupata ufafanuzi wa mada wanazojifunza na mazoezi ya ziada,”amesema.
Silinde amewasihi juu ya kusimamia matumizi na utunzaji wa vitabu hivyo.
“Ni wajibu wenu wasimamizi wa elimu kuhakikisha kwamba vitabu hivyo vinatumika kulingana na utaratibu unaokubalika,”amesema.
Akizungumzia changamoto kubwa katika utayarishaji wa Mitihani ya upimaji ya pamoja katika ngazi za Halmashauri na Mikoa kutokana na tofauti za ukamilishaji wa mada kati ya shule moja na nyingine au kati ya Halmashauri moja na nyingine, Silinde amesema Kalenda hiyo iwe dira mahsusi ya kupanga utaratibu wa kuandaa mitihani ya pamoja kama vile ya ujirani mwema wa shule na Utamilifu.
“Ni matumaini yangu kuwa Maafisa Elimu wa Mkoa kwa kushirikiana na Maafisa Elimu Taaluma mtatumia Kalenda hii wakati wa kuandaa mitihani hiyo ili kupata mitihani inayotokana na mada zilizofundishwa na kukamilishwa katika Shule zote nchini,”amesema.
Amebainisha kuwa Kalenda hiyo itasaidia kupunguza uwezekano wa viongozi wa walimu kulazimishwa kukamilisha mada kabla ya muda uliopangwa.
“Kutokana na majadiliano yenu, imeonekana haja ya kuwa na uchambuzi wa kina wa mawanda ya Kalenda hii kwa kuzingatia hali halisi na tofauti za maeneo yenu ya utekelezaji. Ninatumia fursa hii, kuwaelekeza Maafisa Elimu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa, mnafanya uchambuzi wa kina wakati wa utekelezaji ili muweze kubainisha changamoto na namna ya kuzishughulikia,”amesema.
Amewatoa hofu kuwa kalenda hiyo haitamuondolea mwalimu ubunifu wake wa ufundishaji kama alivyokuwa anafanya kabla ya kuanza kutumia Kalenda hiyo.
Naye, Naibu Katibu Mkuu, TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, amesema Kalenda hiyo imetengenezwa ili kuleta mfanano kwenye utekelezaji wa mitaala nchini na kupima utekelezaji wa mitaala kwa walimu.
“Tumefanya kikao cha siku mbili tumepokea maoni mengi, yakipongeza kazi kubwa iliyofanyika lakini kuna maoni ya kuboresha kazi hii kwa siku zijazo, tunaamini hata tutakapokwenda kutekeleza kuna maeneo yatahitaji maboresho tutaendelea kufanyia kazi, hii ni mara ya kwanza nchini kuwa na kitu hiki,”amesema.
Kwa upande wake, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC), Pauline Nkwama, amesema kalenda hiyo itarahisisha utendaji kazi wa walimu na jamii itafuatilia kwa umakini kinachopaswa kutekelezwa kwa wanafunzi wakiwa shuleni.