MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akiongoza na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa kukagua mradi wa ujenzi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa ujenzi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa Mhandisi wa ujenzi huo wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa ujenzi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatuma Mganga,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa ujenzi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa ujenzi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa ujenzi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
Kiongozi wa Machinga Bw.Bruna Mponzi,akiipongeza Serikali pamoja na uongozi wa jiji la Dodoma kwa kuamua kuwajengea Mradi Mkubwa wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya Mohammed Bulders,Mohammed Halfaj,akielezea mipango waliojiwekea ili kukamilisha ujenzi huo kabla ya wakati.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Mradi wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market linalojengwa katika eneo la Bahi Road Jijini Dodoma ziara hiyo imefanyika leo Januari 13,2022.
…………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kubuni mradi mkubwa wa Soko la wamachinga ‘Machinga Open Market kwa kutumia mapato yake yenyewe huku akiitaka Kampuni iliyopewa mradi huo kukamilisha kwa wakati.
Pongezi hizo amezitoa leo Jumatano Januari 13,2022 Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo ambapo amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kubuni na kuanza ujenzi wa soko hilo katika eneo la Bahi Road Jijini hapa.
Katika ziara hiyo,Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa ameongozana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Fatuma Mganga,Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Joseph Mafuru,Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa,wataalamu kutoka Jiji la Dodoma na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
“Nikushukuru na kukupongeza Mkurugenzi wa Jiji kwa kuchukua hilo wazo wengi wanataka kuona Makao Makuu yanafananaje.Tunaenda kuwa na soko ambalo nchi hii nzima Halmashauri 184 watakuja kujifunza aidha kwa kupenda hata kama ni kimoyomoyo kwamba Jiji la Dodoma limekamilisha mradi huu mkubwa,”amesema
Katika hatua nyingine RC Mtaka ameitaka Kampuni ya Mohammed Bulders kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa mradi huo ifikapo March 17 mwaka huu ili kumpa zawadi Rais Samia Suluhu Hassan ya kutimiza mwaka mmoja tangu awe madarakani.
.“Mnajua sababu ya kutaka Marchi 17 muwe mmemaliza huu mradi ni kwamba siku hiyo Rais atakuwa anatimiza mwaka mmoja akiwa madarakani hivyo nataka tumzawadie zawadi ya hili soko naamini litakuwa ni la kisasa na wamachinga hawakuwa wakipata shida,”amesema.
Mtaka amesema atawashirikisha wataalamu wote kuhakikisha soko hilo linajengwa kisasa na linakuwa na mhaitaji yote ambayo mwanadamu anatakiwa kupata.
“Ndio maana wataalamu wote wapo hapa lengo langu tujenge kitu cha kueleweka hata baada ya miaka kadhaa lakini kubwa nataka Halmashauri zote 184 zije zijifunze hapa namna ya kujenga soko bora la wamachinga hapa kutakuwa na kila kitu na litakuwa soko la saa 24,”amesema.
Aidha amelitaka Jiji la Dodoma mara baada ya Soko hilo kukamilika kuwaondoa wamachinga wote waliopo katikati ya Mji lengo likiwa ni kuliweka Jiji katika hali ya usafi.
“Nategemea mara baada ya kukamilika kwa Soko hili,wamachinga wanaokaa mjini watatupisha na kuja katika hili eneo naamini hapa Mji utakuwa safi na mambo mengine yataenda vizuri,sitegemei soko liwe limekamilika halafu wamachinga wawe wanazagaa mjini,”amesema.
Kwa upande wake,Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Mganga amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kutenga asilimia 40 ya mapato ya ndani kuweza kujenga eneo hilo la wajasiriamali kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7 huku akizitaka Halmashauri zingine za Mkoa huo kuiga mfano wa Jiji la Dodoma.
Hata hivyo ameitaka kampuni ya Mohammed Builders kujenga eneo hilo kwa kiwango ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya kuweka mizigo na kufanyia biashara.
Kwa upande wake,kiongozi kutoka Kampuni ya Mohammed Builders Mohammed Halfaj amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba mradi huo utakamilika muda ambao umepangwa.
“Nikuhakikishie Mkuu wa Mkoa sisi Tutamaliza kazi on time au inshaalah kabla ya ontime,”amesema.
Kwa upande wake,kiongozi wa wamachinga Jiji la Dodoma Bruno Mponzi amelishukuru Jiji la Dodoma kwa kuwashirikisha katika mradi huo ambao amesema watahakikisha wanaofanya biashara katika eneo hilo ni wamachinga na sio watu wengine.
“Tunakiri wazi kwamba tunashirikishwa zaidi nijielekeze kwa mkurugenzi na tumesaidiana wale wanaostahili ndio wanakuwepo.Kutakuwa na watu wanaongezeka lakini kuwe na sifa maalum sio mtu atoke huko, rai kwa wamachinga wenzangu tuwe wazalendo kwa kuhakikisha wale ambao tupo ndio tuwe kipaumbele,”amesema.