Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akioneshwa kiwanja cha Serikali na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akikagua moja kati ya nyumba za Serikali zilizopo Lilongwe, nchini Malawi. Katika ukaguzi huo, Naibu Waziri ameambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiendelea na ukaguzi wa Nyumba ukiendelea
Ukaguzi wa nyumba za Serikali Jijini Lilongwe nchini Malawi ukiendelea
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Mawali na kupokelewa na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati alipofanya ziara katika Ofisi za Ubalozi Jijini Lilongwe, Malawi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimueleza jambo Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba wakati Mhe. Mbarouk alipofanya ziara katika Ofisi za Ubalozi huo Jijini Lilongwe
………………………………………………….
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Ubalozi pamoja na kukagua mali za Serikali nchini humo.
Balozi Mbarouk mara baada ya kukagua mali za Serikali, aliushukuru Ubalozi kwa mapokezi mazuri na kusema kuwa kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kuendeleza kiwanja cha Serikali kwa kujenga jengo la Ubalozi na kitega uchumi.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba amemshukuru Mhe. Naibu wa Waziri – Nje kwa kutenga muda wa kutembelea Ofisi ya Ubalozi na kukagua mali za Serikali zilizopo Lilongwe, licha ya kuwa na ratiba ngumu ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC.