Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama MboniMpaye Mpango wakishiriki Ibada ya Asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Patrick iliopo mtaa wa 11, Lilongwe Nchini Malawi. Januari 11,2022.
……………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama MboniMpaye Mpango wameshiriki Ibada ya Asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Patrick iliopo mtaa wa 11, Lilongwe Nchini Malawi. Januari 11,2022.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini nchini Malawi kuliombea bara la Afrika ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazolikabili. Makamu wa Rais amesema viongozi wa dini wanapaswa kutoa mafundisho yatakayoondoa changamoto za usalama zinazozikabili baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC).
Aidha amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwaombea viongozi wa kisiasa ili waweze kuongoza mataifa yao kwa utashi na hekima na kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi wao.
Makamu wa Rais yupo nchini Malawi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) unaofanyika tarehe 11-12 Januari 2022.