Daniel Udoh alianza kuwafungia wageni dakika ya 27, kabla ya Liverpool ‘kuliamsha dude’ kwa mabao ya Kaide Gordon dakika ya 34, Fabinho mawili, moja kwa penalti dakika ya 44 na lingine dakika ya 90 na ushei na Roberto Firmino dakika ya 78.
Mechi nyingine, Tottenham pia imetoka nyuma na kuichapa Morecambe 3-1 wakati West Ham imeitoa Leeds United.