Mbunge wa Mtambile, Seif Salim Seif (kulia) akimkabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza nahodha wa timu ya Juhudi baada ya kushinda mashindao ya Jimbo. Mbali ya kikombe, timi hiyo pia ilizawadiwa Sh1 milioni.
Mbunge wa Mtambile, Seif Salim Seif (kulia) akimkabidhi jezi na mipira kwa nahodha wa timu ya Mizingani baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Jimbo. Timuhiyo pia ilizawadiwa sh500,000.
Mbunge wa jimbo la Mtambile, Seif Salim Seif (kulia) akimkabidhi mchezaji Hafidhi Ali Maalim wa timu ya Juhudi kiatu chenye thamani ya sh100,000 baada ya kushinda kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Jimbo.
Mbunge wa Mtambile, Seif Salim Seif (mwenye suti) akikagua timu ya Mizingani kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali wa Jimbo Cup kwenye uwanja wa Kengeja, Pemba. Timu hiyo ilifungwa mabao 2-0 na Juhudi na kuzawadiwa Sh500,000, seti ya jezi na mipira mitano.
………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Pemba. Mbunge wa Mtambile, Seif Salim Seif amewazadia washindi mbalimbali wa michuano ya mpira wa miguu ya jimbo yaliyomalizika juzi kwenye uwanja wa Kengeja, Pemba.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya timu 20 ambapo timu ya Juhudi ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuifunga timu ya Mizingani mabao 2-0.
Juhudi FC ilizawadiwa, kikombe, Sh Milioni moja, medali ya dhahabu na mipira 10 kutoka kwa mheshimiwa Seif ambaye ni Mbunge kupitia Chama Cha Wananchi (CUF).
Mbali ya kutwaa kombe, mchezaji Hafidhi Ali Maalim wa timu hiyo alishinda mchezaji bora wa mshindano na kiatu chenye thamani ya sh100,000.
Mheshimiwa Seif pia aliizawadia timu ya Mizingani Sh500,000, mipira mitano na jezi seti moja wakati mshindi wa tatu timu ya Maendeleo ilizawadiwa Sh300,000, jezi seti moja na mipira mitatu.
Mshindi wa nne ni timu ya Warriors ambayo ilizawadiwa Sh200,000, jezi seti moja na mipira miwili huku timu Mtadoda FC ilizawadiwa Sh250,000 na mipira miwili kwa kuwa timu yenye nidhamu.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano hayo, Mheshimiwa Seif alisema kuwa mbali ya kuendeleza mpira wa miguu, mashindano hayo pia yana lengo la kudumisha umoja na kutafuta wachezaji wa kuunda timu ya Jimbo lake ambayo itashiriki katika mashindano mbalimbali.
Alisema kuwa mpaka sasa amevutiwa na wachezaji wengi wenye vipaji ambao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia kiwango cha kuchezea timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
“Malengo yamefanikiwa kwani kupitia mashindano haya, tumeweza kuwa pamoja na kushikamana mbali ya kushindana kupitia timu zetu, nazipongeza timu shiriki, mashabiki na viongozi walioshiriki kufabikisha mashindano haya,” alisema Seif.