MBUNGE Neema Lugangira
MBUNGE Catherine Magige
MBUNGE Lucy Mayenga |
MBUNGE Munde Tambwe
MBUNGE Esther Malleko
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
Katika Historia ya Tanzania haijawahi kutokea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano aanzishiwe mchakato wa kutakwa kujiuzulu na Wabunge wake mwenyewe na zaidi ni Wabunge Wanawake Watano (5) Mashujaa ambao jana tarehe 5 Januari 2022 pia walisimama kidete na kumtikisa Spika Job Ndugai kwa kile walichosema kwamba hawezi tena kuongozo Mhimili wa Bunge maana hakuna tena Mahusiano na Kiongozi wa Mhimili wa Serikali ambae ni Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.
Wabunge hao ni Neema Lugangira, Catherine Magige, Lucy Mayenga, Munde Tambwe na Esther Malleko ambapo kila mmoja kupitia mitandao mbalimbali yakijamii kama instagram, twitter, facebook, na magroup ya whatssup mbalimbali ikiwemo la wabunge ambalo Spika Ndugai mwenyewe alikuwepo humo waliandika kuhusu suala la Spika Ndugai wakitaka awajibike na ajiuzulu huku wakisisitiza wanasimama na Mh Rais Samia Suluhu Hassan.
Pia tarehe 6 Januari 2022 tumeshuhudia Matamko ya Wabunge wengi kutaka Spika Ndugai ajiuzulu na hawa ni pamoja na Mariam Ditopile, Lusinde, Askofu Gwajima, Elly Kingu, na Mrisho Gambo.
Na hivi tunavyoandika leo tarehe 6 Januari,2022 tayari Spika Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu na ikumbukwe hii ni ndani ya Masaa 24 tokea Wabunge Wanawake Watano (5) Mashujaa Neema Lugangira, Catherine Magige, Lucy Mayenga, Munde Tambwe na Esther Malleko, na Lucy Mayenga kutikisa Bunge na Nchi na kusimama na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.