……………………………………..
Na Lucas Raphael
Walimu 368 kutoka mikoa 13 wanaofundisha masomo ya Sanyasi na hisabati katika shule za sekondari nchini wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma kwa kuwapa mbinu za ufundishaji wenye lengo la kuberesha ufaulu .
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu katibu mkuu Elimu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Gerald Mweli wakati akifungua mafunzo ya siku saba jana kwa walimu wa sekondari wanaofundisha masomo ya Sanyasi na hisabati yalifanyika katika shule ya Tabora wavulana mkoani hapa
Alisema lengo ni kuwajengea uwezo, mbinu na umahiri wa ufundishaji na ujifunzaji wa Masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuweza kutoa matokeo chanya kwa wanafunzi.
Alisema kuwa mafunzo hayo ni mahususi katika kuhakikisha walimu wanaweza kuboresha ufundishaji wao hasa katika mada zenye changamoto katika utekelezaji wa Mitaala ya Elimu ya Sekondari.
Alisema, mradi huo umejikita katika maeneo makuu matatu ambayo ni kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya Sekondari, kuweka mazingira wezeshi ya ujifunzaji kwa wasichana na kuwawezesha wasichana na wavulana kukamilisha mzunguko wa Elimu kwa kupata Elimu bora ya Sekondari.
Aidha aliwataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo kwa kuwa wanategemewa kwenda kuwafundisha walimu wengine katika ngazi ya KLASTA kwa lengo la kukamilisha idadi ya walimu 5000 katika mwaka wa fedha 2021/2022.
Awalimu kaimu mkurungezi wa Taasisi ya elimu ya Tanzania ,Moses Ziota alimweleza Naibu kaibu mkuu kwamba mafunzo hayo ni tofauti nay ale ya awali haya yanatumia muundo jumuiya za ufundishaji katika ngazi ya shule na vituo vya ualimu .
Alisema kwamba wawezeshaji wanataopatiwa mafunzo ya awali yatakayoweze kujengea uwezo wa kitaaluma na mbinu za kufundisha na kujifunza ili waweze kutoa elimu kama hiyo kwa walimu wengine katika halmshauri 184 nchini.
Alisema kwamba mradi huo ni endelevu na mafunzo yataendelea kufanyika katika vituo vya mafunzo ya walimu na ngazi za shule yakiwezeshwa na waweeshaji rika .
Ziota alisema kwamba walimu wanaopata mafunzo hayo ni wale wanaofundisha masomo ya Sanyansi na Hisabati ambayo ni Biolojia,Kemia,Fizikia na Hisabati .
Alisema kwamba Tamisemi imeanza kutoa mafunzo hayo kwa washiriki wachache ambao watatumika kama wawezeshaji wa kitaifa katika kuendesha mafunzo endelevu kwa walimu kazini.
Mafunzo haya ambayo yanatekelezwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari ( Sekondary Education Quality Improvement Program-SEQUIP) yanajumuisha washiriki 736 ambapo wamegawanywa katika vituo hivyo viwili (Tabora washiriki 368 na Morogoro washiriki 368 ).