Klabu ya Newcastle United wametuma maombi kwenda Arsenal ili kuipata saini ya Mshambuliaji wa klabu hiyo, Pierre-Emerick Aubameyang, 32, katika dirisha hili.
Mshambuliaji huyo ambaye huenda asionekane tena uwanjani akiwa na jezi ya Arsenal amekuwa hayupo kwenye kiwango bora tangu msimu huu uanze na katika siku za hivi karibuni amevuliwa unahodha kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu.
Newcastle Utd imeripotiwa inataka kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkopo na ndani ya mkataba huo imeweka kipengele cha kumnunua jumla kwa Pauni 20 milioni ikiwa wataridhishwa na kiwango chake.
Dirisha dogo la usajili tayari limeshafunguliwa rasmi nchini England.