Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimina na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono mageuzi ya mfumo wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo mbalimbali yaliyoafikiwa.
Amesema Tanzania itaendelea na mpango wa pili wa Maendeleo wa Msada wa Umoja wa mataifa ambao unatekelezwa sambamba na Dira ya Zanzibar ya 2020 pamoja na awamu ya pili ya mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Taifa (F2016,2021 FYDP2) wenye lengo la kuisaidia Tanzania kufikia Uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 21, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ayefika Ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga Baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa Nchini.
Aidha Makamu wa Rais amemshukuru Bw. Alvaro kwa Ushirikiano na Uhusiano Mzuri alioujenga baina ya Tanzani na Umoja wa Mataifa katika kipindi chake chote alichokuwepo hapa Nchini kwa kusukuma Agenda za Nchi na kuiletea mafaniko katika Sekta mbalimbali na kumtakia kila la heri na kazi njema katika kituo chake kipya cha kazi, ambapo Bw. Alvaro ameteuliwa kuwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Uturuki.
Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwasilisha Taarifa za mapitio ya Hiyari (VNR) ya Utekelezaji wa Maelengo ya Maendeleo Endelevu ya Mwezi Julai 2019 kwa kuwainisha Mafanikio, Changamoto na mbinu bora za kukabiliana nazo pamoja na kujifunza.