Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akipokelewa na wanawawake wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, Wilaya ya Misungwi alipotembelea ofisi za UWT Misungwi leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, Wilaya ya Misungwi, alipotembelea ofisi hiyo leo kwa ajili ya kuzungumza namna bora ya kuinua mapato ya jumuiya hiyo.
Baadhi ya wana Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, Wilaya ya Misungwi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) akizungumza nao katika ukumbi wa UWT Misungwi leo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akikabidhi funguo ya pikipiki kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Misungwi, Bahati Makala ikiwa ni ishara ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya kuanzisha mradi wa bodaboda wa UWT Misungwi ili kuongeza mapato ya jumuiya hiyo. Ameyafanya hayo leo alipotembelea ofisi za UWT Misungwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akikabidhi kompyuta kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Misungwi, Bahati Makala kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya UWT Misungwi alipotembelea ofisi za UWT Misungwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akimkabidhi mtungi wa gesi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Misungwi, Bahati Makala kwa ajili ya wanajumuiya ya UWT Misungwi alipotembelea ofisi za UWT Misungwi leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akikabidhi mitaji ya biashara kwa ajili ya kinamama shilingi milioni saba na laki saba kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Misungwi, Bahati Makala alipotembelea ofisi za UWT Misungwi leo.
***************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa mizinga ya nyuki 50 ili kuunga mkono mradi wa ufugaji nyuki wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Misungwi.
Ameyasema hayo leo alipotembelea Ofisi za UWT Wilaya ya Misungwi ikiwa nimwendelezo wa ziara zake katika mkoa wa Mwanza za kuangalia namna ya kuanzisha miradi katika ofisi za UWT za mkoa huo.
“Kati ya mambo ambayo natamani mfanye ni kuwa na miradi ya kujitegemea na hapa nimesikia mna mizinga ya nyuki mitano, Mwenyekiti ninaahidi nitaongeza mizinga hamsini ambayo itakuwa ni mradi wa UWT hapa Misungwi” Mhe. Masanja amesema.
Pia, Mhe. Mary Masanja amekabidhi fedha za kuwekeza kwenye miradi yenye thamani ya shilingi 14, 650,000 kwa mchanganuo ufuatao;mitaji ya biashara shilingi 7,700,000, mitungi ya gesi 70 yenye thamani ya shilingi 2,800,000, pikipiki moja yenye thamani ya shilingi 2,550,000 na kompyuta moja yenye thamani ya shilingi 1,600,000 kwa kinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, Wilaya ya lengo ikiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Naye, Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Misungwi, Mhe. Angela Gabriel amempongeza Mhe. Mary Masanja kwa kuisaidia jumuiya hiyo.
“Tuna furaha isiyopimika na tumpongeze Mhe. Mary Masanja kwa kuwa mambo anayoyafanya ya kutukabidhi mitaji na majiko ya gesi hayajawahi kutokea katika Wilaya yetu ya Misungwi, tunakushikuru sana” amesisitiza. Mhe. Angela.
Mhe. Mary Masanja yupo Mkoani Mwanza kwa ajili ya ziara ya kutembelea ofisi za UWT mkoani humo kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuanzisha miradi itakayoongeza mapato ya jumuiya hizo.