Mwenekiti mpya wa Halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo aliyekaa katikati wakati wa kikao maalumu kati yao na uongozi wa Tarura Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kujadili mpango wa bajeti hiyo kushoto kwake ni Makamu mwenyekiti na kulia kwake ni Mkurugenzi mtendaji Ramadhani Posi. Mwenekiti mpya wa Halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo wakati wa ufunguzi rasmi kikao hicho maalumu akitoa neno kwa wajumbe wa baraza hilo la madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Posi wa kati kati akiwa anafuatilia mjadala wakati wa kikao hicho kulia kwake ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Dorice Mwakatobe na kulia kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo. Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu kupitia titeti ya chama cha mapinduzi (CCM) alizungumza jambo katika kikao hicho. Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa baraza hilo wakiwa wameketi kwa ajili ya kusikiliza na kuchangia katika kikao hicho.
Mwonekano wa baaadhi ya viongozi wa Tarura kutoka Wilaya ya Bagamoyo wakiwa wanafuatilia kwa ukaribu jinsi ya mwenendo mzima wa kikao hicho la baraza la madiwani.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
********************************
NA VICTOR MASANGU, CHALINZE
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwa pamoja limepitisha mpango wa makadirio kwa bajeti ya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya miundombinu ya barabara za vijijini kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi kufikia 2023.
Hayo yamebainishwa na Mwenekiti mpya wa Halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo wakati wa kikao maalumu kati yao na uongozi wa Tarura Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kujadili mpango wa bajeti hiyo ambayo inatarajiwa kuanza utekelezaji wake kwa mwaka 2022 katika miundombinu ya barabara hasa zilizopo maeneo ya vijijini.
Mwenyekiti huyo alisema kuna baadhi ya maeneo mbayo ni kiofi sana hadi wakati mwingine wananchi wenye mazao yao mashambani wanashindwa kwenda kuyachukua kutokaka na kuwa na barabara mbovu hivyo mpango huu tumeweza kuupitisha kwa pamoja na madiwani wenzangu ili uweze kuanza kazi kwa lengo la kuwasaidia wananchi wetu.
“Mpango wa Rais wetu mpendwa ni kuendelea kutoa fedha kwa lengo la kuwez a kutengeneza miundombunu ya barabara hasa katika maeneo ya vijijini na kwamba tuna imani kazi hii pindi itkapoanza itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa wananchi ambao walikuwa wanasumbuka kubeba mazao yao mashambani.”alisema Mwenyekiti huyo.
Pia aliongeza kuwa katika halmashauli ya Chalinze kuna maeneo mengi ambayo yamekuwa ni chachu katika kuwaingizia kipato hivyo yatanakiwa kuguswa na Tarura ili yaweze kufunguka kwa kiasi kikubwa na kuendelea kutoa fursa za kufikika kwa urahisi ili kuongeza uchumi kwa wanachalinze pamoja na Taifa kwa ujumla
Mwenyekiti huyo aliwaasa wananchi wote wa Chalinze na maeneo mengine ya jirani kujenga tabia yaa kuitunza miundombinu ya barabara ambayo inajengwa na kuwataka Tarura wafanye kazi kwa ushirikiano na kuzingatia maelekezo ambayo ameyatoa Rais Samia Suluhu ya kuwahudumia wananchi kwa kuwapelekea huduma hiyo.
Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Bagamoyo Mhandisi Emmanuel Ndyamukama amebainisha kwamba kwenye mfuko wa barabra wametengewa kiasi cha shilingi milioni 744 na lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanazitumia kwa mujibu wa miongozi waliopatiwa katika kutengeneza na kufanya ukarabati wa miundombinu ya barabara zilizopo katika halmashauri ya Chalinze pamoja na Bagamoyo ikiwa ni kuboresha huduma zaidi kwa wananchi wote
“Lengo letu ndugu Mwenyekiti wa halmashauri ni kuwekaa mipango madhubuti kwa ajili yaa kuwafikia wananchi sambamba na hilo ni kuwasogezea huduma iliyo bora katika suala zima la kuunganisha mtandao wa barabara zilizopo katika maeneo yaa Bgamoyo ili ziweze kupitika kwa urahisi kutokana n hali halisi ya mahitaji ambayo yanahitajika kwani serikali imeweza kutoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo,”alifafanua Meneja huyo.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu kupitia titeti ya chama cha mapinduzi (CCM) amesema kwamba anatarajia kuona mabadiliko makubwa pindi utekelezaji wa mpango huo wa Tarura ukianza utekeelzaji wake katika kuwafikishia upatikanaji wa huduma pindi barababar hizo zitakapotengenezwa na kuweza kupitika kwa urahisi hasa wanapokwenda kupata huduma za matibabu pamoja na mambo mahitaji mengine ya msingi.
“Mimi Kama Mbunge natumani yangu makubwa mapendekezo ya bajeti hii kwa wananchi wa chalinze pindi itakapoaanza kutekelzwa basi kutakuwa na maendeleo makubwa sana kwa njia zetu ambazo zilikuwa na changamoto ya kupitika zitaweza kupitika kwa urahisi na kwamba nawapongeza uongozi wa Tarura kwa kuletaa mapendekezo haya pamoja na baraza zima la waheshimiwa madiwani kwa kukubaliana na kutoa maoni yao kwa pamoja ili kazi iweze kuanza hapo mwakani,”alifafanua Mgalu.
Pia Mgalu akusita kumshukuru na kumpongeza Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti kwa tarura kwa ajili ya kuwawezesha wataalamu waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ya kuboresha miundombinu ya barabara katika halmashauri ya Chalinze pamoja na halmashauri ya Bagamoyo.
Kwa upande wake Kaimu katika Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Dorice Mwakatobe aliwataka wataalamu wa Tarura kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao ipasavyo kulingana na yale yote ambayo wameyapendekeza na kuyaazimia katika kikao hicho cha baraza la madiwani ili kuweza kuwaletea chachu ya maendeleo wananchi wote.
Katika hatua nyingine aliwaomba viongozi wa Tarura kuyachukua mapendekezo yote ambayo yametolewa katika baraza hilo la madiwani kwa kuweza kuyafanyia kazi kwa weledi lengo ikiwa ni kutimiza malengo yote ambaayo wamejiwekea na kukubaliana kwa pamoja ili utekelezaji wa bajeti ukianza kufanyika hapo mwakani kuwe na mwelekeo wa matokeo chaya katika miundombinu ya barabara.
Nao baadhi ya madiwani ambao wameshiriki katika kikao hicho wameiomba Tarura kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha zaidi miundombinu ya barabara iweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote hasa katika njia za kuelekeaa katika huduma mbali mbali za kijamii ikiwem, sekta ya faya. Elimu, kilimo pamoja na maeneo mengine.