**************
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa anaungana na watanzania wote kumpongeza Rais wa Jamhuri ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Aftika (SADC).
Magufuli amerithi mikoba ya kiti cha Uwenyekiti wa SADC kutoka Kwa mtangulizi wake Rais wa Namibia, Dr. Have Geingob na atadumu na cheo hicho Kwa mwaka mmoja.
Makonda amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kumpa pongezi Magufuli kutokana na kuaminiwa Kwa utendaji wake wa kazi.
“Kwetu Sisi tunaona fahari Kwa kiongozi wetu kupewa jukumu la kuongoza nchi 16 zilizo ndani ha SADC ni matokeo ya uzalendo nasi tunapaswa kuendeleza uzalendo Kwa vitendo.
“Tuna jukumu la kuendeleza uzalendo ambao uliachwa na Mwalimu Julius Kambarange Nyerere ambaye ni mmoja wa waasisi wa Jumuiya hii kwa kuwasaidia wengi kupata Uhuru, hatuna bundi kuungana na kiongozi wetu ambaye Kwa sasa ana jukumu la kuendeleza Yale yaliyoachwa na waasisi hasa malengo yake makubwa yamekuwa ni kutotoa kwenye Lindi la umaskini.
“Kama ambavyo amesema kuwa Mataifa yetu si maakini na namna jitihada zilivyotumika kuwatoa wengi kwenye utumwa hizo ndizo zitatumika kuyatoa Mataifa yetu kwenye dimbwi la umaskini kama alivyosema kwenye hotuba yake, ni wakati wetu wa kuungana na kumpa sapoti,”.