……………………………………………………….
Na Asila Twaha, Kongwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa yapokea shilingi milioni 250 zinazotokana na tozo za miamala ya simu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Chitego kilichopo Kata ya Chitego.
Hayo ameyabainisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo alipokuwa ameambatana na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho na kueleza kuwa mbali ya Kata ya Chitego kuwa ni eneo la kimkakati kutokana na shughuli za kiuchumi na uwepo wa watu wengi lakini kwa huduma za Afya Kata hiyo wananchi wake walikuwa wanafuata huduma mbali.
Ameendelea kwa kueleza Kata ya Chitego ilikuwa haina kabisa Kituo cha Afya na watu hufuata huduma hospitali ya Wilaya takribani kilometa 100 na kwa Kituo cha Afya cha jirani ni zaidi ya kilometa 40 ambapo ni Kata ya Mkoka.
“Naishukuru ya Serikali Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha hizi za tozo za miamala ya simu ambazo ni mkombozi kwa wananchi wa Kata ya Chitego kwa kupata kituo cha Afya kama ambavyo Kata hii ipo pembezoni mwa mpakani mwa Mkoa wa Manyara” amesema Dkt. Omary
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chitego Peter Kalunzu amesema wamepata changamoto nyingi sana ikiwemo wamama kujifungua njiani kutokana na kufuata huduma mbali za hospitali amesema kuwa kwa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo itawasaidia wananchi kupata huduma kwa karibu.