…………………………………………………
Happy Lazaro, Arusha
Arusha. Jeshi la polisi Jijini Arusha linamshikilia Patrick Mmasi (24) mkazi wa Njiro, jijini hapa, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi ,Ruth Mmasi (40)ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini
na kisha mwili wake kuutumbukiza kwenye chemba la choo katika nyumba yake.
Tukio la aina yake limegundulika baada ya raia wema kutoa taarifa za Siri Polisi ambao walikwenda na kubaini mwili huo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari amesema taarifa rasmi zitatolewa kesho.
Hata hivyo Masejo amethibitisha polisi kumshikilia Mmasi kwa tuhuma za kifo cha utata cha Ruth Mmasi ambaye katika.uhai wake alikuwa mfanyabiashara wa madini.
“Tunamshikilia kijana huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani na taarifa rasmi itatolewa”amesema
Taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu zinasema tukio hilo liligundulika juzi baada ya Polisi kufika nyumbani kwa marehemu kufanya upekuzi na kubaini mwili ukiwa ndani ya chemba ya choo.
Kwa mujibu wa ndugu huyo ,mtoto wa marehemu Patricia Mmasi (19) anayesoma Nchini China, alipata mashaka akiwa china wakati alipojaribu kumpigia simu mama yake Ruth na simu yake kutopatikana kwa muda wote.
Amesema aliamua kusafiri kuja Tanzania kwa sherehe za Xmass na kumuuliza kakaye Patrick kuhusu kutoonekana kwa mamayake na kutopatikana kwenye simu, ambapo kijana huyo alikuwa akimjibu kuwa kwani mama yako akiondoka huwa ananiaga??? ndipo yeye na ndugu wengine wakaamua kutoa taarifa Polisi.
Aliongeza kuwa Polisi walipofika walifanya upekuzi katika sehemu mbalimbali za nyumba hiyo ya kisasa yenye ghorofa moja na ndipo wakabaini mwili huo ukiwa ndani ya chemba la choo nyuma ya nyumba hiyo na mwili huo umegundulika baada ya siku 14 ukiwa ndani ya chembe hiyo.
Ndugu huyo alidai kuwa marehemu alikuwa akiishi na kijana wake huyo ambaye ndiye Mtoto wake wa kwanza na mara nyingi walikuwa wakitofautiana .
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa mwili huo ulikuwa umeanza kuharibika na umehifadhiwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru Kwa uchunguzi zaidi.
Kwa Mujibu wa ndugu marehemu Ruth atazikwa nyumbani kwao kesho alasiri katika eneo la Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara.
Wakati huo huo polisi wameonya watu katika kipindi hiki cha siku k kujihusisha na uhalifu kwani Ulinzi umeimarishakatika Maeneo mbalimbali ya Jiji.