Aliyeko katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya LG Afrika Mashariki,Sa Nyoung Kim akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Arusha leo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Benson Ltd , Nadeem Hussein akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo jijini Arusha leo.
Aliyeko kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya LG Afrika Mashariki,Sa Nyoung Kim wakikata utepe kwa pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Benson Ltd,Nadeem Hussein(kulia) ishara ya uzinduzi wa duka hilo jipya jijini Arusha leo.
************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Wananchi na mkoa wa Arusha na mikoa jirani wametakiwa kutumia fursa katika msimu huu wa sikukuu ya kununua bidhaa zilizo bora na zenye viwango vikubwa ambazo ni rafiki kwa mazingira .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji kampuni ya vifaa vya LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka jipya la vifaa vya LG kwa kushirikiana na Kampuni ya Benson lengo likiwa ni kuwasogezea huduma karibu wateja wao vikiwa na viwango na ubora wa hali ya juu.
Kim amesema kuwa,kwa zaidi ya miaka 41 Sasa kampuni ya Benson wamekuwa wauzaji wakuu wa bidhaa za kampuni ya LG mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwasogezea huduma kwa karibu wateja wake.
Kim amesema kuwa,hiyo ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo ya LG kuzindua duka hilo mkoani Arusha baada ya kuzindua maduka mengine matatu jijini Dar es Saalamu mwaka huu lengo likiwa ni kusambaa Tanzania nzima.
“Bidhaa hizi tulizozindua hapa leo ni TV za kisasa,friji ,mashine za kufulia nguo ambapo vifaa hivyo vimetengenezwa kisasa zaidi na zinatumia umeme mdogo sana na tunaahidi wateja wetu kuwa miezi michache ijayo tuna mpango wa kufungua maduka mengine ya LG katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuwapatia huduma wateja wetu”amesema Kim.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa bidhaa za umeme ya Benson Ltd ,Nadeem Hussein amesema kuwa,wamekuwa wakitoa huduma zilizobora na za uhakika kwa wateja wao katika kuuza bidhaa zinazomgusa kila mtu .
Nadeem amempongeza Rais Samia kwa namna ambavyo amefungua fursa za kufanya biashara katika nchi mbalimbali na hivyo kupanua wigo wa wafanyabiashara kufanya biashara kwa Uhuru bila kusumbuliwa na mtu yeyote.
“bidhaa zetu tunazouza zina ubora wa hali ya juu na zinapunguza matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa Sana ,na pia gharama zetu zinamfanya mteja yotote kuweza kununua , hivyo tunawaomba wateja wajitokeze kwa wingi kuja kununua .”amesema Nadeem.
Meneja wa duka la LG Benson Arusha,Zahra Mohamed amesema kuwa,bidhaa hizo zina manufaa makubwa sana kwani ni rafiki kwa mazingira na ni za kisasa na wametoa punguzo la bei kwa asilimia 20 kwa bidhaa zao zote katika msimu huu wa sikukuu ili wateja waweze kupata huduma hizo kwa urahisi zaidi.