Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga,akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa kilichofanyika leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa,akizungumza kwenye kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa kilichofanyika leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma .
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM,Gilbert Kalima,akielezea malengo ya kikao hicho wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa kilichofanyika leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma .
Katibu wa Organization CCM Taifa,ambaye ni Mlezi wa Jumuiya za chama hicho,Dk.Modeline Castica,akizungumza wakati kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa kilichofanyika leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma .
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dk. Philis Nyimbi, akizungumza wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa kilichofanyika leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma .
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa kilichofanyika leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma .
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi kimewaonya watu walionza kupanga safu ya viongozi kabla ya muda wa uchaguzi wa ndani ya chama na jumuiya zake unaotarajiwa kufanyka mwaka 2022 ambapo ni kinyume na maadili ya chama hicho .
Onyo hilo limetolewa leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo kwenye ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Wazazi ambapo amesema kuwa uchaguzi wa ndani ya chama na jumuiya zake utafanyika mwakani 2022.
Kanali Lubinga amesema mwaka 2022 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani ya chama na jumuiya zake uchaguzi maana yake ni mfumo wa kijamii ya kistaarabu kupata uongozi,kuendesha jumuiya na kwa lugha ya kisiasa ni sehemu ya kidemokrasia.
Pia Kanali Lubinga amesema chama kina imani uchaguzi huo utaendeshwa kwa ustaarabu na kanuni za Chama na Jumuiya lakini kampeni zake bado muda na ukifika wataariwa na wote ni lazima wazifuate.
“Iko minongono miongoni mwenu mmeanza kupiga kampeni hii ni kinyume cha maadili ya chama chetu na Jumuiya,Kibaya zaidi tunasikia watu wanabeba viongozi na wengine wameisha anza kutoa rushwa na kupokea ni vema ukaacha wala usithubutu hakuna kisichofahamika.
“Simu yangu inazo Whatsup zenye ushahidi na Katibu Mkuu wetu wa CCM anahafamu yote chama kimelazimika kufanya mabadiliko ya viongozi kutokana na mwenendo usioridhisha na hakitasita kuchukua hatua,”amesema Kanali Mstaafu Lubinga
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa amesema Jumuiya imejipanga kulipa madeni mbalimbali ambayo wamekuwa nayo pamoja na kushughulikia migogoro ya mipaka ya shule zake.
“Kutoka sasa kila fedha tutakazipata tutatoa parcent na kuweka fungu la kulipa madeni haiwekekani tunasemwa huko nje hatulipi madeni tuna wastaafu wetu tuna wajane tuna mazungumzo na Serikali hili lifanyike,”amesema.
Naye,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Gilbert Kalima amesema wataendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha makusudia yanayohitajika ndani ya Jumuiya yanafikiwa.
Kwa upande wake,Katibu wa Organization CCM Taifa,ambaye ni Mlezi wa Jumuiya za chama hicho,Dk.Modeline Castica amewashukuru viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo kwa kusimamia mambo mbalimbali ikiwemo katika chaguzi mbalimbali za Ubunge na Udiwani.