……………………………………………………..
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imefanikiwa kuvuka lengo la kupanda miti kwa zaidi ya asilimia 83,ikiwa ni mpango mkakati wa Serikali kuungana na Jumuiya ya kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi.
Hayo yameelezwa na Afisa Maliasili anayesimamia uhifadhi rasilimali mazingira katika Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga wakati wa mahojiano maalumu kuhusu hatua zinazochukuliwa na Halmashauri hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia-Nchi.
Amesema Mpaka sasa Halmashauri hiyo imepanda miti laki tatu na themanini kati ya laki sita na hamsini iliyokusudiwa kupandwa katika msimu wa mvua za Vuli, wakati lengo kuu ni kupanda miti Milioni moja na hamsini katika kipindi cha msimu wa mvua za masika.
“Lakini sisi kama Manispaa mpango tulionao tunataka kuondoa changamoto ya upatikanaji wa miti lakini kukabiliana na changamoto za mazingira mvua chache na changamoto zingine kingine nikuhakikisha miti inawafikia wananchi lakini pia kuna shule nne tayari zimepata ufadhiri wa kuotesha miti kwa ajili ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa miti kwa wananchi”.
Ametoa wito kwa Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuzingatia matumizi endelevu ya nishati mbalimbali kama hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ,na kwamba suala la uhifadhi wa Mazingira ni jukumu la kila mmoja.
“Bado tunaendelea kutoa wito kwamba matumizi endelevu ya nishati ikiwemo gesi matumizi ya maji, matumizi ya kila siku ya nyumbani usafi suluhisho moja la kudumu ni wananchi kufikia mahara wakaelewa changamoto tuliyonayo na wakamuunga mkono mheshimiwa Rais ambaye ameshiriki na kusaini makubaliano ya uhifadhi ya misitu mabadiliko ya tabia nchi yanawagusa moja kwa moja wananchi na wala siyo serikali peke yake serikali kazi yake ni kutengeneza sela ambazo zitatatua changamoto lakini Shinyanga ni wahanga wa mabadiliko ya tabia nchi”.
Kwa upande wao Wananchi wameahidi kushiriki vyema kwenye suala la uhifadhi wa mazingira kama hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.