Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Iringa na wakandarasi wakati wa ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo katika halmashauri ya wialaya ya Iringa
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya ya
Iringa na wakandarasi wakati wa ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo
katika halmashauri ya wialaya ya Iringa
Moja kati ya madaraja ambayo yanaendelea kujengwa katika barabara za halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Moja kati ya madaraja ya watembea kwa miguu ambayo yanaendelea kujengwa katika barabara za halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Na
Fredy Mgunda,Iringa
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga ameridhirishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa ya Uviko 19 na kuziagiza Halmashauri zote kuhakikisha miradi yote mipya
ya ujenzi wa majengo inakamilisha ndani ya siku 60 pekee
Akiwa
katika Ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa, Halmashauri ya
Wilayani ya Iringa Sendiga alisema kuwa kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo iwe
chachu kwa Halmashauri na wakandarasi kukamilisha miradi ya maendeleo kwa
wakati.
RC
Sendiga aliupongeza uongozi wa wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Iringa kwa
kusimamia vilivyo hadi kukamilisha kwa wakati miradi hhiyo ya ujenzi wa
madarasa ya fedha za UVIKO 9.
Alisema
kuwa madarasa hayo yamekamilika kila kitu kilichobaki ni kuwasubili tu
wanafunzi waanze kuyatumia kipindi ambacho watakuwa wanaanza mwaka wa masomo.
ziara
hii ya mkuu wa mkoa wa Iringa imejiri ikiwa ni Wiki Kadhaa zimesalia kabla ya
muda uliotolewa na Serikali kukamilishwa kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa
yanayojengwa kwa msaada wa fedha za uviko 19
Alisema
kuwa amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa huku
akiwahakikishia wananchi kuwa vyumba hivyo vitakamilika kwa wakati na
viutatumika kwa masomo hapo mwakani
Katika
Ziara hiyo Mkuu huyo wa mkoa pia amekagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na
madaraja na kutoa muda wa wiki mbili kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa
daraja la Tosamaganga kabla ofisi yake haijamchukulia hatua.
RC
Sendiga alisema kuwa hafurahishwi hata kidogo na kasi ya ujenzi wa daraja la
Tosamaganga kwa kuwa mkandarasi wa daraja hilo yupo nje ya mkataba nab ado
hajakamili ujenzi na kupelekea adha kubwa kwa wananchi ambao wamekuwa
wanalitumia daraja hilo.
Aidha
Sendiga pia amekagua ujenzi wa barabara pamoja na daraja la lilopo katika
barabara ifunda, bandabinchi linalogharimu zaidi ya milioni 984 ambapo
amelidhishwa na ujenzi wa daraja hilo pamoja na barabara hiyo.
Alitumia
muda huo kumpongeza injinia wa Wakala wa barabara mjini na Vijijini Wilayani
Iringa Barnaba Jabiry kwa kazi nzuri ya usimamizi wa daraja na barabara hiyo.
Kwa
upande wake Injiania wa Wakala wa barabara mjini na Vijijini Wilayani Iringa
Barnaba Jabiry amelitaja daraja hilo kuwa mkombozi kwa wakazi wa kata takribani
3 wilayani humo.
Alisema
kuwa daraja hilo likikamilika litakuwa mkombozi wa shughuli za kiuchumi kwa
wananchi wa kata hizo tatu za Tarafa ya Kiponzero na nje ya Tarafa hiyo kwa
kukuza maendeleo
Naye
mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wafanyakazi wa
Halmashauri ya wilaya ya Iringa wamefanya kazi kubwa kuhakikisha miradi ya
madarasa ya fedha za UVIKO 19 yanakamika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa
kitaifa na kimataifa.
Alisema
kuwa mkurugenzi na wataalam wake wamekuwa hawapumziki kila uchwao wapo
barabrani kuhakikisha miradi ya ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati
kama ulivyokuwa umepangwa.
Moyo
alisema watendaji hao wamefanya kazi kubwa ya kusimamia miradi mbalimbali ya
kimaendeleo katika Halmashuri hiyo na hawapaswi kuvunjwa mioyo yao kwa
kuwakatisha tama wakati wa usimamizi wa miradi hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu
ya sita kwa kutoa fedha za kutekeleza ujenzi wa miradi ya barabara na madaraja
katika jimbo hilo ambalo awali kulikuwa kuna kero nyingi kwa wananchi juu ya
daraja hilo ambalo litatumiwa na zaidi ya kata tatu za Tarafa ya Kiponzero.