CHUO cha Teknolojia ya Reli Tanzania kimekusudia kuongeza udahili wa wanachuo hadi kufikia 1,000 ifikapo mwaka wa masomo wa 2023/24.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Chuo hicho Damas Mwajanga wakati wa mahafali ya kwanza ambayo yamejumuisha wahitimu 137 katika fani mbalimbali.
Alisema lengo kuongeza udahili ni kuongeza Wataalamu katika mbalimbali ambao watasaidia katika kuchochea maendeleo ya usafishaji kwa njia ya reli ikiwemo kumudu matumizi reli ya mwende kazi.
Mwajanga alisema utekelezaji wa mpango huo unazingatia agenda ya Afrika ya mwaka 2063 inazingatia kuchchea mageuzi ya kiteknoojia na kibiashara barani Afrika.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda amelitaka Shirika la Reli Tanzania(TRC) kuhakikisha linatoa kipaumbe kwa Wahitimu wa Chuo na Wakufunzi katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka Dodoma kupitia Tabora hadi Mwanza.
Alisema hatua itasaidia kupanua ujuzi walioupata na kuwaongezea mbinu wakufunzi za kuendelea kutoa elimu bora kwa wanachuo ambao bado wako masomoni.
Katika mahafali hayo ya kwanza ya Chuo hicho wahitimu 46 wametunukiwa Stashahada ya Awali ya Usafishaji, 34 Astashahada ya Awali ya Usafishaji,20 Astashahada ya Awali ya Teknolojia ya Matengenzo ya Njia ya Reli na 37 Astashahada ya Ukuaguzi na Matengenezo ya Mabehewa.