………………………………………………………………
Mashindano ya 11 ya Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyokuwa yakifanyika Jijini Arusha yamemalizika huku Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikishinda vikombe nane.Timu zilizoibuka washindi wa jumla na kuwa Mabigwa ni pamoja na;
· Timu ya Mpira wa Miguu
· Timu ya Mpira wa Pete (Netball)
· Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) Wanaume
· Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) Wanawake
· Timu ya Mpira wa Kikapu ( Basketball) Wanaume
· Timu ya Mpira wa Kikapu ( Basketball) Wawake
· Timu ya Kuvuta Kamba Wanaume
· Timu ya Riadha Wanawake
Aidha katika mashindano mingine Timu za Bunge la Tanzania zimeibuka Washindi wa Pili katika michezo ifuatayo;
· Mchezo wa Kutembea kwa kasi Wanawake-Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson aliibuka Mshindi wa Pili.
· Mchezo wa Kutembea kwa kasi Wanaume-Mbunge wa Nungwi, Mhe. Simai Hassan Sadik aliibuka Mshindi wa Pili
· Timu ya Kuvuta Kamba Wanawake waliibuka Washindi wa Pili
· Mchezo wa Darts Timu ya Wanaume wallibuka Washindi wa Pili.
Michezo ya Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilihusisha Timu kutoka Mabunge 6 ya Tanzania, Kenya, Burundi, Zanzibar, Sudan Kusini, Uganda na Bunge la Afrika Mashariki ambao walikuwa wenyeji.