MKURUGENZI wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Andrew Komba,akishiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
Meneja msaidizi maendeleo ya rasilimali misitu (TFS) kanda ya kati Patricia Manonga,akipanda miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe zoezi lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Sebastian Warioba,akishiriki kupanda miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
Viongozi pamoja na wadau mbalimbali wakiendelea na zoezi la kupanda miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Andrew Komba,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kushiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Afisa wa Maji Ofisi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Bi.Felisiana Mpanda,akielezea umuhimu wa kupanda mti wakati wa zoezi la kupanda miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Sebastian Warioba,akizungumzia lengo la kupanda Miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira lililofanyika leo Desemba 18,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKURUGENZI wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Andrew Komba, amewata wananchi kutumia kipindi hiki cha mavua za masika kupanda miti ili kurejesha uoto wa asili na kukabilina na mabadiliko tabianchi.
Hayo ameyasema leo Desemba 18 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la vyanzo vya maji Mzakwe lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira.
Dk.Komba amesema kuwa ni muhimu mikoa yote nchini kujiandaa na zoezi la upandaji miti katika kipindi hichi cha mvua za masika ili kukabiliana na mabadiliko tabianchi.
“Sisi kama serikali pamoja na wadau wa mazingira tutahakikisha kuwa zoezi la upandaji miti linakuwa endelevu”amesema Dk. Komba
Aidha Dk.Komba amesema kuwa wananchi wanao wajibu wa kuhakikisha kuwa wanalinda vyanazo vya maji kwa kuacha kufanya shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo hayo.
Amesema kuwa Ofisi yake itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya hifadhi za maji ambayo watu wamekuwa wakivamia na kufanya shughuli za kibinadamu.
“Serikali za maeneo husika zichuke hatua kali kwa watu ambao wamekuwa wakijihusha na matukio ya uharibifu wa vyanzo vya maji kama vile ukatai miti ovyo na uchomaji wa misitu”amesema
Kwa upande wake Meneja msaidizi maendeleo ya rasilimali misitu (TFS) kanda ya kati Patricia Manonga, amesema kuwa miti waliyopanda katika eneo hilo ni zaidi ya 1,000.
“Miti hii tunayopanda hapa imefanyiwa utafiti kutokana na eneo hili kujaa maji wakati wa masika na miti ambayo tumipanda ni ile ambayo ni rafiki na inatunza vyanzo vya maji”amesema Manonga
Hata hivyo, amewataka wananchi kutumia nishati mbadala ili kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo ni chanazo kikubwa katika uharibifu wa mazingira.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Sebastian Warioba amesema kuwa eneo hilo la hifadhi ya maji Mzakwe ndiyo tegemeo kuu la maji katika jiji la Dodoma.
Bw.Warioba amesema kuwa lengo la kupanda miti katika eneo hilo ni kusaidia kurejesha hali ya uoto wa asili ambao umeharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu.
“Eneo hili kama manavyoliona limechomwa moto na watu ambao wamekuwa wakijihusisha ma uwindaji ambao siyo rasmi na kusababisha miti yote ambayo alipanda Rais Samia Suluhu Hassan wakati ule akiwa makamu wa Rais mwaka 2017”amesema Warioba