Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,akizungumza wakati akifungua kikao cha siku moja cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga,akijibu hoja mbalimbali wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akizungumza kwenye kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo,akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Mkuu wa wilaya wa Dodoma,Jabir Shekimweri,akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remedius Emmanuel ,akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe,akitoa taarifa ya utekelezaji wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili mbaga,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,akijibu hoja mbalimbali wakati wa kikao cha siku moja cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
Washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha siku moja cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jijini Dodoma
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,amesema kuwa kuna haja ya wakandarasi wa ndani ya Mkoa kushirikishwa kwenye miradi mikubwa ili kuwajengea uwezo.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha siku moja cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Dodoma ambapo amesema kuwa hatua hiyo itaongeza uwezo na ujuzi wa wakandarasi wa ndani ya Mkoa.
Mtaka amesema kuwa umefika wakati Wakandasi wa Mkoa kuwashirikisha katika miradi hiyo inayotekelezwa ili waweze kujengewa uwezo mkubwa wa kufanya kazi hizo.
” Kuna miradi mikubwa inayotekelezwa mkoani Dodoma, mfano barabara za ring road, Kuna ujenzi wa reli ya kisasa ambayo inatekeleza na wakandarasi wakubwa sana, hivyo kuna haja ya kuwa engage(kuwashirikisha) wakandarasi wa ndani ya mkoa hata kwa sub-contact ili tuweze kuwajengea uwezo”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa amesema kuwa kuna changamoto kwenye barabara za Mkoa wa Dodoma hususani za wilayani na kuzitaka TANROADS na TARURA kuangalia namna kuzishughulikia.
” Mbali na barabara pia kuna madaraja mawili ya Gulwe na Godegode ambayo yanasumbua sana mfano Daraja la Godegode limetengenezwe na kuharibika, kumekuwa na malalamiko sana ya wananchi ya ubovu wa barabara na haya madaraja ambayo yanaharibika kila wakati.”
Amesema wakati wanasubiri ujenzi wa kudumu wa madaraja hayo, ni vyema yakajengwa madaraja wa muda ambayo yataimarisha Mawasiliano hasa wakati wa kuelekea mvua nyingi. Wakala wa Barabara umetenga Sh bilioni 1.5 Kwa ajili ya matengenezo ya daraja korofi la Godegode.