Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakari Kunenge akiwa katika halfa hiyo ya makabidhiano ya gari lakubebea wagonjwa kwa wananchi wa kata ya Kibindu.
**************************
Na Victor Masangu,Chalinze
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amekabidhi rasmi gari kwa ajili ya kituo Cha afya Kibindu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa wa kuwasaidia wananchi kutembea umbari mrefu hususan wakinamama wajawazito.
Kunenge amekabidhi gari Hilo la wagonjwa katika halfa fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi za halmashauri ya Chalinze na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,madiwani,madakrari pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Issa.
Katika halfa hiyo Kunenge aliupongeza kwa dhati uongozi wa halmashauri ya Chalinze kwa kuona umuhimu wa kuboresha sekta ya afya kwa kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa gari hilo la wagonjwa.
“Kwa kweli Mimi Kama Mkuu wa Mkoa kwa hatua hii nichukue fursa ya kipekee kuwapongeza viongozi wote wa halmashauri chini ya Mkurugenzi kwa kufanya maamuzi sahihi katika kununua gari hili ambalo litakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa kata ya Kibindu na maeneo mengine ya jirani,”alisema Kunenge.
Aidha aliziagiza halmashauri zote tisa kuhakikisha wanatenga bajeti kupitia mapato yao ya ndani kwa ajili ya kununua magari hayo ya kubebea wagonjwa ili wananchi waweze kuondokana na adha ya kutembea umbari mrefu kufuata huduma.
Alifafanua zaidi Kunenge alisema kwamba kwa Sasa unatakiwa kuwa na magari yapatayo 38 lakini yaliyopo kwa Sasa ni 22 hivyo kuna upungufu wa magari 18 ambayo yanahitajika kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.
Katika hatua nyingine alieleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha wanaboresha huduma ya afya kwa wananchi kwa kuendelea kujenga zahanati,vituo vya afya,nyumba za wauguzi pamoja na madaktari.
“Inapaswa halmashauri zetu tisa zilizopo katika Mkoa wa Pwani ziongeze nguvu zaidi katika ukusanyaji wa mapato ambayo yatawasaidia kujiendesha wao wenyewe pamoja na kuisaidia serikali katika suala zima la utoaji wa huduma kwa wananchi,”alisema Kunenge.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Issa aliongeza kuwa kupatikana kwa usafiri wa gari hilo kutakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata ya Kibindu ambao walikuwa wanateseka kutembea umbari mrefu wa kilometa 200 kutoka makao makuu ya Wilaya.
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Kibindu akiwemo Amina Almasi alimpongeza Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wake kwa kuwatengea fedha kwa ajili ya miradi mbali mbali ikiwe afya.