Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira uliomalizika leo Desemba 17,2021.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira uliomalizika leo Desemba 17,2021.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Maafisa wa Afya Tanzania (CHAMATA),Twaha Mubarak,akizungumzia waliyojifunza katika mkutano ho wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira uliomalizika leo Desemba 17,2021.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima (hayupo pichani), wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira uliomalizika leo Desemba 17,2021.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima akimpongeza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Maafisa wa Afya Tanzania (CHAMATA),Twaha Mubarak, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira uliomalizika leo Desemba 17,2021
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima,akikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa mashindano ya taifa ya usafi wa mazingira kwa mwaka 2021 mara baada ya kufunga kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira uliomalizika leo Desemba 17,2021.
……………………………………………………………….
Na Alex Sonna, Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima amesema wastani wa wagonjwa sita kati ya 10 wa nje wanaohudhuria katika vituo vya kutolea huduma za afya wanasumbuliwa na magonjwa ambayo yangedhibitiwa kwa njia ya usafi wa mwili na mazingira.
Kufuatia hali hiyo, ameagiza kuanzia sasa kila nyumba iliyopo na itakayojengwa kuhakikisha inakuwa na choo bora kitakachotumika muda wote na si cha maonyesho ya bwana na bibi Afya.
Dk.Gwajima ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira.
“Sote tunatambua kwamba maradhi yanayotokea mara kwa mara kwa jamii yetu yanauhusiano wa moja kwa moja na utaratibu duni wa usafi na usalama wa maji na mazingira na hivyo kusababisha uchafuzi wa vyakula na vinyaji na kueneza maradhi kama kuharisha, kipindupindu, homa za matumbo, ini na minyoo,”amesema.
Amehimiza kufanyika kwa kaguzi za mara kwa mara kwenye maeneo yote yanayozalisha vyakula ili kudhibiti magonjwa hayo.
“Mara kadhaa tunaelezwa na watafiti na pia kupitia taarifa mbalimbali za kiutendaji zinazoonesha kwamba sehemu kubwa ya matatizo ya kiafya tunayoshughulika nayo ni yale ambayo yanaweza kuzuilika kwa njia ya usafi wa mazingira,”amesema.
Waziri huyo amesema serikali imedhamiria kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wote wa sekta ya afya nchini ikiwamo wataalamu wa afya ya mazingira.
Ili kutimiza malengo hayo, amesema Wizara imepanga kununua magari na vitendea kazi kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Maafisa Afya Mazingira nchini.
Kadhalika, amesema serikali imeandaa mwongozo wa uwekezaji katika taka ngumu ili kuhamasisha uwekezaji na kuongeza jitihada za kuboresha usimamizi wa taka hapa nchini.
Ameahidi kufanyiwa mapitio kwa Sheria ya Afya ya jamii kutokana na kupitwa na wakati ili ikidhi mahitaji ya sasa.
Akitangaza matokeo ya mashindano ya taifa ya usafi wa mazingira kwa mwaka 2021, Mkoa wa Manyara, Katavi na Dodoma zimeibuka kinara wa usafi.
Kwa upande wa Halmashauri za Majiji ni Tanga, Arusha na Mwanza, huku Manispaa ya Moshi, Iringa na Kinondoni pia zikifanya vizuri.
Miji ni Njombe, Tunduma na Babati na kwa upande wa Halmashauri za Wilaya ni Njombe, Makete na Moshi.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk Ntuli Kapologwe amesema wataalamu wa afya mazingira wataongezwa ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwamba upandishaji madaraja kwa watumishi ambao bado utafanyika kwakuwa maelekezo yalishatolewa.