Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akisisitiza umuhimu wa Wakurugenzi wa Halmashauri zinazonufaika na mradi wa timiza ndoto zako Mei 25, 2019 Wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Mukunda akizungumza wakati wa hafla ya kuzunduliwa kwa mradi wa timiza ndoto yako Wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akisisitiza jambo kwa Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuzindua mradi wa timiza ndoto zako.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Mhe. Oscar Mukasa akizungumza katika hafla ya kuzinduliwa kwa mradi huo.
Sehemu ya wanafunzi na wazazi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa timiza ndoto zako wakifuatilia uzinduzi huo Wilayani Bahi.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa timiza ndoto zako.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) Bw. Koech Rotich katika hafla ya kuzindua mradi wa Timiza ndoto yako Bw. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huo Wilayani Bahi.
Sehemu ya wanufaika wa mradi wa Timiza ndoto zako wakitoa shuhuda za mafunufaa wanayopata kupitia mradi huo na kupongeza Serikali kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi huo
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaonufaika na mradi wa timiza ndoto zako wakitoa ushuhuda wa faida za mradi huo .
Mbunge wa Bahi Mhe.Omary Baduel akisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mradi wa timiza ndoto zako kutumia mradi huo kujikwamua na kujiletea maendeleo.
Na Mpiga picha wetu
………………..
Na.Alex Sonna,Bahi
SERIKALI imezindua mradi wa miaka mitatu wa timiza malengo kwa wasichana wa rika balehe walioko shuleni na wanawake vijana waliopo mitaani utakao saidia kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika kijiji cha Chikola wilayani Bahi mkoani Dodoma, Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi nchini (Tacaids) Dk. Leonard Maboko, amesema kuwa mradi huo ni wa majaribio katika mikoa mitatu na Halmashauri 10 nchini.
Dk.Maboko amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwawezesha wasichana walio katika lika balehe waliko shuleni pamoja na wanawake vijana walioko mitaani ili waweze kuondokana na vishawishi vitakavyo wasababishia kupata maambukzi ya virusi vya ukimwi.
Aidha amesema kuwa katika mradi huo utawasaidia wasicha katika rika balehe, kuweza kupata fedha kila ambazo zitawaondoa katika vishawishi na wanawake vijana kupata shughuli za uzalishaji mali.
“Katika mradi huu jumla ya walengwa 15,954 wasichana walio shuleni watanufaika kwa kupata fedha Sh. 25,000 kila mwezi kwa miaka mitatu ambazo zitawasaidia kujikimu katika mahitaji mbalimbali ikiwemo kujinunulia tauro laini wakiwa katia kipindi chao cha hedhi na mahitaji mengine ya shule ”amesema Dk. Maboko.
Hata hivyo amesisitiza kuwa pia wanawake vijana waliopo mitaani 14,295 walio nje ya shule watanufaika kwa kufundishwa stadi za maisha ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa biashara ndogondogo ambazo zitawasaidia kijikimu ili kuweza kuepukana na maambuki ya mapya ya Vvu.
“Wanafundishwa na kuandaa mpango wa biashara kwa kusaidiawa na maafisa ugavi na akiwasilisha huo mpango napatiwa asilimia 60 ya fedha na baadaye anamaliziwa asilimia 40 iliyobaki, kiasi chenyewe cha fedha ni Sh.400,000 ambacho siyo haba katika mtaji wa biashara kwani kuna watu walianza na 10,000 lakini leo wanamamilini”amesema
Dk. Maboko amesema kuwa mradi huo umekuja kutokana na takwimu kuonyesha maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi katika umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24 ni asilimi 40 huku kati yao wasichana ni asilima 80 ya maambukizi yote.
“Hivyo basi kutokana na ukubwa wa takwimu hizi ndipo tukaamua kuanzisha mradi huu ambao utawawezesha wasichana kuondoka na changamoto hii pia tuweze kufika zile 90 tatu ifikapo 2030”alisisitiza
Akitoa ushuhuda kuhusu walivyonufaika na mradi huo Mmoja wa wanafunzi ya shule ya msingi Chikola Wilayani Bahi Maria Severin, amesema kuwa toka kuanza kwa mradi huo umewezesha kuongeza mahudhulio shuleni kutokana na kupata mahitaji yote.
“Tunaishukuru serikali yetu kwa mradi huu kwani hivi sasa tunashiriki vipindi wakati wote kutokana na kupatiwa fedha kiasi cha Sh, 25,000 kila mwezi ambazo tunazitumia kununua mahitaji yetu mbalimbali hali inayotusaidia kuepukana na vishawishi mitaani”amesema
Kwa upande wake mmoja wa wazazi wa wanafunzi aliyenufaika na mradi huo Bi.Mayasa Mussa amesema kuwa wanafunzi wamefurahia mradi huo na kuwapa moyo wa kwenda shule imeongezeka kwani kila mwezi watapokea elfu 25,00 kwa kila mwezi na kuwawezesha kukidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi hao ikiwemo kupata taulo za kike,sare za shule na mahitaji mengine
Mradi huo wa Timiza ndoto zako unatekelezwa katika mikoa mitatu na Halmashauri kumi ukilenga kuwawezesha wasichana waliobalehe wakiwa mashuleni na wale walio nje ya mfumo wa elimu.