Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akisisitiza jambo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akizungumza katika kikao cha kuwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. White Zuberi,akichangia wakati wa kuwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
Mjumbe wa Halmsahauri Kuuu CCM Mkoa wa Dodoma Bw.Ahidi Sinene ,akichangia mada wakati wa kuwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
Wakuu wa wilaya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu jijini Dodoma.
…………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKOA wa Dodoma umewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu.
Akiwasilisha taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,amesema kuwa Mkoa huo umekusanya mapato ya zaidi ya Sh. bilioni 21.955 sawa na asilimia 35 ya makisio ya kukusanya zaidi ya Sh. bilioni 64.069 zilizopangwa kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Mtaka amesema kuwa Mkoa unaendelea kufanya jitihada za kuongeza makusanyo ya mapato yake ili kupanua shughuli za maendeleo.
Amesema kati ya Bajeti ya mwaka 2021/22, mkoa umekisiwa kukusanya Sh. 64,069,966,000 ambapo hadi hufikia Novemba 2021 Sh. 21,954,702,178.37 zilikuwa zimekusanywa sawa asilimia 35.
Mtaka amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/21 Sh. 27,416,259,808 zilitegwa na kutolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zote.
Hata hivyo ameeeleza kuwa katika Bajeti ya 2021/22 makasio ya mapato ni Sh. 64,069,966,000 ambapo Sh. 42, 339, 858,025 zinatarajiwa kutengwa kwa ajili ya shughulimza maendeleo.
“Hivyo kwa kipindi cha Januari hadi Novemba Sh. 37,131,924,765 zilitolewa na halmashauri zote kwa ajili ya shughuli za maendeleo”amesema
Amesema kuwa mwezi Novemba Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa maendeleo ya taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 ambapo Mkoa wa Dodoma ulipatiwa Sh. 17,667,017,106.40 hivyo kufanya Bajeti ya Mkoa kuwa Sh. 359,334,353,456.40.
Mtaka amesema katika fedha zilizotengwa zimewezesha kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwamo madarasa ya shule za msingi na sekondari, ujenzi wa maabara na matundu ya vyoo ya zahanati na vituo vya afya, majengo ya Utawala, utengenezaji wa madawati uimarishaji na ukusanyaji mapato na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
”Mpaka Novema 2021, mikopo ya Sh 5,818,392,313 zilitolewa sawa na asilimia 97 ya lengo la kutoka Sh. bilioni 6 huku vikundi 461 vikinufaika na mikopo hiyo vikihusisha vikundi 282 vya wanawake, 136 vya vijana na 43 vya watu wenye ulemavu”amesema Mtaka