Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Allan Kijazi, akifunga mafunzo ya namna ya kufanya maeneo yenye sifa za kipeke katika nchi za Afrika kuingia kwenye orodha ya urithi wa Dunia, Jijini Ilala Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Malikale nchini Dkt Christowaja Ntandu akiongea katika ufungaji wa mafunzo ya namna ya kufanya maeneo yenye sifa za kipeke katika nchi za Afrika kuingia kwenye orodha ya urithi wa Dunia, Jijini Ilala Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, akimpatia cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya namna ya kufanya maeneo yenye sifa za kipeke katika nchi za Afrika kuingia kwenye orodha ya urithi wa Dunia, Jijini Ilala Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Urithi wa Dunia Afrika (AWHF) Bw Souyibou Varissou
*********************
Na Sixmund J. Begashe
Wizara ya Maliasi na Utalii nchini, inatarajia kuyaingiza maeneo mengi yenye sifa za kipeke na yaliyobeba urithi adhimu wa historia, kwenye Urithi wa Dunia ili yaweze kuvuta watalii wengi, kutoa fursa za ajira na kuchangia katika pato la Taifa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Allan Kijazi alie wakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga kwenye ufungaji wa Mfunzo ya namna ya kufanya maeneo yenye sifa za kipeke katika nchi za Afrika kuingia kwenye orodha ya urithi wa Dunia.
Dkt Kijazi awapongeza washiriki wote wa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kuesema kuwa mafunzo hayo na mengine yanaendana na malengo ya kimkakati ya Mfuko wa Urithi wa Dunia Afrika (AWHF) unaolenga kuendeleza Urithi wa Dunia kwa Nchi Wanachama Barani Afrika.
“Mafunzo haya yamewakutanisha kwenye meza moja wataalam, wasomi wanaosimamia Urithi wa Utamaduni na Malikale, rasilimali hii inaujuzi na uzeofu mbukwa juu ya michakato ya Urithi wa Dunia na pia wanauelewa mpana juu ya Mkataba unaotuongoza”. Dkt Kijazi
Kaimu Mkurugenzi wa Malikale nchini Dkt Christowaja Ntandu, amesema Afriaka inamaeneo mengi amabayo ni yaasili na utamaduni laini ni machache sana ambayo yapo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia hivyo kwa kupitia mafunzo hayo ipo nafasi kubwa kwa wataalam kuandaa mafaili na maeneo mbalimbali yanayoweza kupendekezwa kuingia katika urithi wa Dunia.
“Baada ya mafunzo haya wataalam wetu sasa watakaa na kuanza mchakato wa kutambua na kuandaa maadiko ya kupendekeza maeneo yenye sifa za kipekee ambazo zitawezesha kuingia kwenye oridha ya Urithi wa Dunia, na Tanzania tunamaeneo mengi ambayao tunaweza kuyaingiza katika orodha hiyo”. Dkt Ntandu
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Urithi wa Dunia Afrika (AWHF) Bw Souyibou Varissou amesema zipo nchi wanachama za Afrika ambazo hazina eneo hata moja kwenye orodha ya Urithi wa Duni, hivyo amewashauri wataalam hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuungana ili kuhakikisha nchi zote zinakuwa na maeneo hayo ili kuvutia watalii kwa wingi, kutoa ajira na uelewa mpana wa umuhimu wa maeneo hayo.
Mratibu wa Mafunzo hayo DKT James Wakiba amesema kuwa nchi takribani saba, zimeudhuria mafunzo hayo ikiwemo Tanzania, ambazo zimewasilisha maeneo yao yaweze kuchakatwa kitaalam ili kukidhi kuingizwa kwenye orodha ya Urithi wa Dunia.