Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiteta jambo na Balozi wa China nchini Wang Ke.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Balozi wa China nchini Wang Ke zawadi ya picha inayoonesha baadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi za Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China.
…………………..
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 61 wakitanzania kwa mwaka huu.
Akizungumza katika sherehe za kuwaaga wanafunzi hao katika eneo la Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam, Prof.Ndalichako amesema kuwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zote mbili kati ya Tanzania na China utakuwa ni ushirikiano endelevu.
Aidha, Prof.Ndalichako ameiomba Serikali ya China kuweka utaratibu wa ufadhili kwa wakati mwingine uwe kwa wahandisi wa umeme hasa kutokana na mradi wa ujenzi wa Reli kukamilika hivi karibuni.
“Tunaomba kuwepo na ufadhili katika masuala ya usafiri kwa ujumla hasa reli kwa kutambua kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli anaendelea kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge kwahiyo tungependa kuwa na mainjinia ambao watakuja kuendesha mradi huo pindi utakapokamilika”. Amesema Prof.Ndalichako.
Pamoja na hayo Prof.Ndalichako amewapongeza wanafunzi waliochaguliwa kupata nafasi ya ufadhili wa masomo nchini China na kuwashauri waweze kutumia nafasi hiyo vizuri ili kuweza kupata ujuzi na maalifa ili baadae waweze kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wanaongeza kasi ya kujenga uchumi nchini.
“Mkawe mabalozi wazuri katika nchi yetu,mnakwenda China mtakutana na watu wa China pia mtakutana na watu wa mataifa mengine ambao wengine hawajawahi kufika nchini Tanzania kwahiyo kielelezo chao ni matendo yenu,tabia zenu na mwenendo wenu, nawaomba sana vijana msiende kutengeneza jina baya”. Ameongeza Prof.Ndalichako.