Watendaji mbalimbali wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Tanzania bara na Zanzibar wakitoa elimu katika Mwalo wa Kayenze Wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya ziara ya Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoani humo.Mialo ni sehemu mojawapo ambayo kumekuwa kukiripotiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na mwingiliano wake na shughuli ambazo zimekuwa zikifanyika (Picha zote na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)