Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Komredi Ramadhani Maneno akiwa katika ziara ya kikazi visiwani Mafia.
***********************
Na Victor Masangu,Pwani
Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Komredi Ramadhani Maneno amewataka madiwani kuhakikisha kwamba wanasimamia fedha vizuri zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
Maneno ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika Visiwa vya Mafia yenye lengo la kuzungumza na wanachana wa CCM pamoja na kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayotekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama.
Alisema kwamba lengo lake ni kuona fedha ambazo zinatolewa na serikali zinakwenda kutekeleza miradi kwa maslahi ya wananchi hivyo viongozi na madiwani katika maeneo yao husika no vema wakawajibika ipasavyo katika suala zima la fedha.
Kadhalika Mwenyekiti huyo akieahimiza watendaji kujenga tabia ya kuwa mshikamano pamoja na uwajibikaji wa hali ya juu katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao mbali mbali ya kila siku.
“Nimefanya ziara yangu ya kichama katika Visiwa vya Mafia na nimetembekea miradi mbali mbali ya maendeleo lakini kitu kikubwa ni kuwa na mshikamano wa pamoja kwa watendaji wote pamoja na madiwani ili tuweze kuwaletea wananchi wetu maendeleo,”alisema Maneno.
Katika ziara hiyo ya siku tatu ambayo imeweza kuleta mafanikio makubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Mafia pamoja na viongozi wa Chama na serikali ikiwa na lengo la kuweza kujionea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika sekta tofauti.
Mwenyekiti huyo wa CCM ameweza kufanya mikutano yake katika maeneo mbali mbali ikiwemo Tarafa za Mafia Kusini na Kaskazini ikiwemo mikutano ya ndani kwa wanachama wake.