Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu,akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) nchini Bi. Shalini Bahuguna,akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Tigest Katsela Mangestu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri,akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Masuala ya Afya; Mhe Dkt Festo Dugange,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga,akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki pamoja na watoto wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,(hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akiwa na watoto wakizundua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,amezindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) huku akiwataka wadau wote kushirikiana katika utekelezaji mpango huo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma Dk.Gwajima amesema kuwa baada ya uzinduzi wa programu kazi iliyobaki ni utekelezaji wake.
“Program hii inafungua milango kwa sekta zote pale zinapotaka kumuandaa Mtanzania wa kesho zitapitia kwenye programu hii na kuhakikisha mtoto huyu anaandaliwa vizuri”amesema Dkt. Gwajima
Dkt. Gwajima amesema ili MMMAM iweze kuwa na tija inahitaji kuwanufaisha watoto wote kwa usawa hasa wale wanaoishi na kufanya kazi Mitaani kuweza kurudi kwenye mfumo Rasmi ili waandaliwe kwa usalama wa Taifa la baadaye.
Hata hivyo amesema kuwa utafiti wa hali ya lishe uliofanywa na Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Mwaka 2018, ilibainika kuwa, zaidi ya watoto 2,600,000 chini ya miaka mitano Tanzania wamedumaa.
“Idadi kubwa wakiwa katika Mikoa 11 ambayo ni Dar-es-Salaam, Kagera, Kigoma, Mara, Dodoma, Geita, Tanga, Ruvuma, Mbeya, Morogoro, na Tabora”amesema
Aidha,Dk.Gwajima amesema zaidi ya watoto 270, walio chini ya umri wa miaka mitano nchini Tanzania hupoteza maisha kutokana na matatizo yanayohusiana na lishe duni.
Pia Dk.Gwajima amewataka wazazi kuwafuatilia kwa karibu watoto wao kwani suala la ujifunzaji unaanza tu mara anapozaliwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Wizara itaendelea kuratibu na kusimamia kupungua kiwango cha utapiamlo na udumavu pamoja na kusimamia Mifumo ya ulinzi na usalama wa mtoto.
Dkt Jingu amesema Program ya MMMAM ilianza kuandaliwa mwaka 2019 ikiwa ni sehemu ya maazimio ya kikao Cha Wadau wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto.
Naye Mwakilishi mkazi wa Shirika la kimataifa la watoto linalojihusha na masula ya watoto UNICEF Shalin Bahuguna alisema watashirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa programu hiyo inafanikiwa ili kuwa na taifa bora