Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akimsikiliza Ofisa Mawasiliano na mahusiano wa Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) Symphrose Makungu mara baada ya kutembelea na kukagua banda hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akiipongeza Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) mara baada ya kutembelea na kukagua banda hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akionyeshwa kitabu kinachotumika kufundishia watoto na Ofisa Mawasiliano na mahusiano wa Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) Symphrose Makungu mara baada ya kukagua banda hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) imepongezwa kwa kuzalisha wataalamu wa Malezi na Makuzi ya awali ya Watoto pamoja na kutoa wataalamu wa kusimamia Mpango huo.
Hayo yamesemwa leo Desemba 13,2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jiinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima wakati wa uzinduzi wa programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto (PJT-MMMAM) uliofanyika jijini Dodoma
Akizungumza katika banda la maonyesho la KTO, Waziri Dk Gwajima amesema uzinduzi wa programu hiyo una maana kubwa lakini akasifia namna taasisi hiyo inavyofanya kazi kwa kuzalisha wataalamu wa Malezi na Makuzi ya awali ya Watoto.
Amesema kutoa huduma bila kuwa na malengo ya mbele haitakuwa nzuri lakini kuzalisha wataalamu ni jambo la msingi kwa mustakabali wa siku za mbeleni.
“Kufundisha wataalamu wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ni jambo nzuri sana, nimelipenda, naamini kuwa wanaofundishwa watakuwa chachu ya kuzalisha watu wenye uelewa na faida kwa nchi,” amesema Dk Gwajima.
Naye Ofisa Mawasiliano na mahusiano wa KTO Symphrose Makungu amesema kwa kutambua umuhimu wa Malezi ya mtoto, taasisi yao ilianza kutoa elimu katika vyuo 10 nchini nchini ambako wanaendelea kuzalisha watoa elimu Vijijini.
Makungu amesema wanatoa elimu hiyo katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii (FDs) vilivyoko katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambako hadi sasa washiriki 125 wamefuzu hivyo wanaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Wizara itaendelea kuratibu na kusimamia kupungua kiwango cha utapiamlo na udumavu pamoja na kusimamia Mifumo ya ulinzi na usalama wa mtoto.
Dkt Jingu amesema Program ya MMMAM ilianza kuandaliwa mwaka 2019 ikiwa ni sehemu ya maazimio ya kikao Cha Wadau wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto.
Kabla ya uzinduzi, kulikuwa na mafunzo ya mpango huo yaliyowashirikisha waandishi wa habari za watoto, Waganga wakuu wa mikoa na Maofisa wa elimu kutoka mikoa mbalimbali nchini.