Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza Jambo wakati wa ziara hiyo.
…………………………………………………………….
Na Victor Masangu,Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge katika kuboresha sekta ya elimu ameiasa jamii kuwapeleka shule watoto wa kike na kuwaacha wasome mpaka mwisho kwa manufaa yao pamoja na Taifa kwa ujumla ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea.
Kunenge aliyasema hayo alipofika kukagua ujenzi wa madarasa saba kwenye Kituo shikizi katika kitongoji cha Zoladendeni Kijiji cha Kisegese wakati wa ziara yake mbali mbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Kunenge alitembelea na kukagua miradia ya maendeleo ambayo inayojumuisha katika sekta za Miundo Mbinu ya Elimu iliyopatiwa fedha za mpango wa Taifa wa mapambano dhidi ya Uviko-19 iliyopo katika Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza katika kituo hicho, Kunenge aliwataka wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwa usawa bila ya kuwa na ubaguzi wa kijinsia bali wawawezeshe wote kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao.
“Kikubwa ninachowaomba walezi na wazazi kuhakikisha wanawawekea misingi mizuri watoto wao hasa wa kike ili kuweza kuwapa fursa ya kuwapeleka shule lengo ikiwa ni kupata elimu kwa manufaa yao wenyewe na Taifa kwa ujumla,”alisema Kunenge
Aidha Kunenge alibainisha kuea Msangapwani ni kituo shikizi kilichoanzishwa mwaka 2018 kikiwa na wanafunzi 80 na ni miongoni mwa vituo vilivyopata fedha za madarasa saba yenye thamani ya shilingi milioni 140.
Katika ziara yake hiyo pia Kunenge aliweza kufanya UKAGUZI wa mradi wa ujenzi wa madarasa (19) yenye thamani ya kiasi Cha shilingi milioni 380 katika shule ya sekondari Vikindu.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara alikagua na kuridhishwa na uwekaji matuta kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam – Lindi kwenye eneo lililokuwa hatarishi kwa wakazi wa Kimanzichana.
Kadhalika alipata fursa ya kunionea maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Vikindu – Sangatini yenye urefu wa kilomita 18.65 inayounganisha na Wilaya ya Kigamboni inayojengwa kwa kiwango cha Lami kwa thamani ya shilingi milioni 499.7.
Aliongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo ambao unasimamiwa chini ya usimamizi wa TARURA kwa Sasa maendeleo yake yanakwenda vizuri na kwamba kwa Sasa umefikia kiwango cha asilimia 85.