Mkutano wa 21 wa Baraza la
Mawaziri la Kisekta

 (BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

 katika ngazi
ya Makatibu Wakuu unafanyika leo

 tarehe 9 Desemba 2021katika Hotel Verde mjini

 Zanzibar.

 

Mkutano huu na mkutano wa ngazi
ya Maafisa

 Waandamizi ambao ulifanyika tarehe 6 hadi 8

 Desemba 2021 ni sehemu
ya mikutano ya awali

 yenge jukukumu la kupitia na kuwasilisha agenda

 na
mapendekezo ya masuala ya afya ya kikanda

 yatakayowasilishwa katika Mkutano wa 21
wa

 Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya

 ya Afrika Mashariki
utakaofanyika tarehe 10

 Desemba 2021.

 

Ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huu

unaongozwa na Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu  Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 

Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia – Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto  wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mkutano huu unafanyika mjini
Zanzibar
kwa lengo la kuendeleza jitihada za jumuiya katika kutangaza maeneo ya utalii
ndani 
ya jumuiya. Vilevile kuvutia wageni na kuhamasisha utalii wa ndani kama ilivyosisitizwa katika maonesho ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-Tourism Expo) yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021  Jijini Arusha.

==============================

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma H. Mrisho (Kulia) akifuatilia Mkutano wa 21 wa Baraza  la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo tarehe 9 Desemba katika Hotel Verde mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota.

Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu, kutoka Kenya, Dkt. Moses Mbaruku (kati) akiongoza mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe. Chrisophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi kutoka Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kenya, Dkt. Kuria Francis.

Ujumbe wa Tanzania 

Ujumbe wa Tanzania

Ujumbe wa Tanzania

Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania

Ujumbe kutoka Kenya

Ujumbe kutoka Uganda

Ujumbe kutoka Burundi